Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
February 6, 2025 at 12:38 PM
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) yenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya ardhi. Kikao hiko kimefanyika Februari 06, 2025 makao makuu ya Umoja huo jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa UWT, Mary Pius Chatanda na Makamu wa UWT, Zainab Khamis Shomari.

Comments