
Wizara ya Ardhi
February 8, 2025 at 07:29 AM
WASHIRIKI WARSHA YA KUANDAA MPANGO KAZI WA UANZISHWAJI MFUMO WA NSDI WATEMBELEA KITUO CHA TGNC
Washiriki wa Warsha ya Kuandaa Mpango Kazi wa Uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (NSDI) wametembelea Kituo cha Ubunifu na Mafunzo ya Kijiografia (TGNC) kilichopo (UDOM) jijini Dodoma Dodoma.
Wakiwa katika kituo hicho washiriki hao ambao ni wataalamu kutoka Taasisi za serikali na sekta binafsi walipata maelezo kuhusiana na kituo cha TGNC sambamba na kutembelea maeneo ya chuo kwa lengo la kujifunza.
Warsha ya uandaaji Mpangokazi wa uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (National Spatial Data Infrastructure- NSDI) ilianza Februari 3, 2025 na kumalizika Februari 7, 2025.