
Wizara ya Ardhi
February 15, 2025 at 12:48 PM
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameongoza Kikao cha baraza la madiwani na Kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya ya Kiteto pamoja na wataalamu wa Ardhi wa Mikoa ya Dodoma na Manyara Februari 15, 2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara kujadili migogoro ya Ardhi iliyopo Wilayani humo kabla ya Mkutano na wananchi wa Wilaya hiyo utakaofanyika katika kijiiji cha Ndareta.