
Wizara ya Ardhi
February 20, 2025 at 11:57 AM
OFISI YA ARDHI KIGOMA YAANZA ZOEZI LA NYUMBA KWA NYUMBA KUKUSANYA MADENI YA KODI LA PANGO LA ARDHI
Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Kigoma imeanza zoezi la kutembelea nyumba kwa nyumba katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa lengo la kuwafikia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi ili kuhakikisha malengo ya makusanyo ya maduhuli ya serikali yanafikiwa.
Zoezi hilo linahusisha maafisa wa ardhi wanaotembelea wamiliki wa ardhi wenye malimbikizo ya madeni kwa ajili ya kuwakumbusha wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati, huku hatua za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa dhidi ya wale watakaoshindwa kutekeleza.
Kwa mujibu wa maafisa wa ardhi, mkakati huu unalenga kuongeza mapato ya serikali na kuimarisha matumizi bora ya ardhi kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla. Wakazi wa Kigoma Ujiji wamehimizwa kushirikiana na maafisa wa ardhi ili kufanikisha zoezi hilo.