Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi
February 24, 2025 at 07:37 PM
Wananchi wa Morogoro Wahimizwa Kulipa Kodi ya Pango la Ardhi na Kuhakikisha kupata Kibali cha Ujenzi Wananchi wa mkoa wa Morogoro wamehimizwa kulipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati na kuhakikisha wanapata kibali cha ujenzi kabla ya kuanza ujenzi kwenye viwanja vyao. Wito huo umetolewa wakati wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kuhusu huduma za ardhi zinazotolewa mkoani humo, ikilenga kuongeza uelewa na kufuata taratibu za kisheria katika umiliki na maendeleo ya ardhi. Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa kufuata sheria za ardhi ili kuepuka migogoro .

Comments