KISHIMBA_TV
KISHIMBA_TV
February 19, 2025 at 05:59 PM
NAMUNGO FC (0️⃣) vs (3️⃣) SIMBA SC. 🔴Kipindi cha kwanza Namungo Fc Wamecheza na Simba sc kwa nidhamu kubwa wakifahamu simba wanahitaji alama tatu muhimu, wakaamua kuwaacha simba wacheze mpira na wao kutumia counter attacks kwa kushtukiza wakiwa wametimia ile kadi nyekundu ilibadilisha mchezo. 🔴Walifunga njia zote za kumfikia golikipa wao na mipira mingi ilikuwa inaishia kwenye eneo la ulinzi la Namungo Fc, Tatizo lao lilikuwa wapo Busy sana na Refa wakiamini kila tukio wanaonewa hawakujua wanatoka mchezoni zimetoka. Sana kadi za njano za kumzonga muamuzi. 🔴Simba wametumia Fullback kushambulia ili mawinga waongeze wingi kwenye Boksi la Namungo lakini hakuna kilichofanikiwa hakuna short on target hata moja kipindi cha kwanza penalty ndo ilitengeneza utofauti wa mechi. 🔴Kipindi cha pili mechi kwa upande mmoja ni Namungo kupokea mashambulizi shimo limepatikana kwa kadi nyekundu ikawa tuzuie tusifungwe nyingi. Moussa Camara Cleansheet 15🔥 JEAN AHOUA MIPIRA YA KUTENGA🔥 HAMZA “Spear” UTULIVU 👑🔥 NAJIM MUSA DK 30 za mwanzo kacheza vizuri🔥 MAN OF THE MATCH👑 Hamza Spear Jr ana mchezo mzuri anaenjoy soka sana.

Comments