
KISHIMBA_TV
55 subscribers
About KISHIMBA_TV
NEWS, ENTERTAINMENT &SPORTS⌚️ ✍️Story za Kweli Na Uhalisia✍️..
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars inashuka dimbani hii leo kumenyana na Equatorial Guinea kusaka nafasi ya kufuzu WAFCON 2026, mchezo huu utapigwa majira ya saa 10 jioni kwenye dimba la Azam Complex. Kila la Kheri Twiga Stars.🔥

TAARIFA. 🚨🌍 VAR itatumika kwenye Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kuanzia robo fainali hadi fainali.

*Simba kukutana na Al Masry ya Misri.*🔥🔥 Kama unaamini *Ubaya Ubwela* lazima uonekane weka 👍 na kama unaamini safari ya Simba imeisha weka 😂 hapa👇

Twiga Stars wanashinda mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania nafasi ya kufuzu WAFCON 2026, pale Azam Complex Chamazi na sasa wapo mguu ndani kuelekea mchezo wa marudiano kule Equatorial Guinea. WAFCON 2026 QUALIFIERS; FT: Tanzania 🇹🇿 3️⃣-1️⃣ 🇬🇶 Equatorial Guinea ⚽️Stumai Abdalah ⚽️Enekia Kasonga ⚽️Diana Msewa

ROBO FAINALI YA MOTO: SIMBA SC vs AL MASRY *Uchambuzi mfupi:* Simba SC wanakuja na kasi na faida ya uwanja wa nyumbani, huku Al Masry wakitegemea nidhamu na uzoefu wao wa kimataifa. Simba SC:Wanategemea mashambulizi ya kasi na ubora wa viungo wao katika kutengeneza nafasi. Al Masry: Wanajivunia safu imara ya kiungo na ulinzi thabiti, lakini wanapaswa kuwa makini na kasi ya Simba. Wachezaji wa kuangaliwa: Simba SC:Kibu Denis – mshambuliaji mwenye nguvu, kiboko wa Waarabu, hatari anapokuwa kwenye boksi. Simba SC:Ahoua - mmoja wa vinara wa kutengeneza nafasi za mabao, kiungo mwenye macho ya pasi za mwisho. Al Masry:Fakhreddine Ben Youssef– mshambuliaji mwenye uzoefu, anayejua kufunga katika mechi kubwa. Takwimu za Al Masry dhidi ya Simba kwenye CAF CC: 🗓️Machi 7, 2018 Simba 🇹🇿 2️⃣ - 2️⃣ Al Masry ⚽️ 9' Bocco (P) ⚽️ 11' Ahmed ⚽️ 25' Abdalraof ⚽️ 74' Okwi (P) 🗓️ Machi 17, 2018 Al Masry 🇪🇬 0️⃣ - 0️⃣ Simba 🇹🇿 Nani ana nafasi kubwa? Simba SC wanaweza kutumia faida ya uwanja wa nyumbani na kasi yao, lakini Al Masry wanaweza kutumia uzoefu wao kuzuia mashambulizi. Ushindi utategemea umakini wa safu ya ulinzi na ubunifu wa viungo katika kutengeneza nafasi. "Mchezo wa mpira ni hesabu, anayekosea anaadhibiwa!.

Kule nchini Qatar mjini Doha majira ya saa 11 jioni inafanyika droo ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho huku Simba SC ndio wawakilishi pekee waliyosalia kwenye michuano hiyo. Simba anaweza kukutana na wapinzani kati ya hawa: ➡️Stellenbosch ➡️ASEC Mimosas ➡️Al Masry