AjiraCoach Platform
February 26, 2025 at 03:28 PM
*MAONI BINAFSI KUHUSU AJIRA ZA WALIMU*
*Utangulizi.*
Binafsi naipongeza secretariat ya ajira Kwa kusimamia zoezi la usahili vizuri kwani ni Jambo geni kwetu na kwao pia Katika kada hii. Zipo hoja ambazo naungana na walio wengi ambazo ndizo za msingi na baadhi nazani sio za msingi kwani zinatugawa Kwa kigezo cha umri na mwaka wa kuhitimu.
*Changamoto nilizozibaini Kwa taasisi.*
1\. Nafasi za ajira ni chache ukilinganisha idadi ya walimu walio mtaani. Hivo inafanya baadhi ya watu kutokua na imani na mchakato. Mfano Angalia somo la Kiswahili IIIC kati ya walioomba, walioitwa kwenye usahili na waliofanya usahili wa kuandika, utagundua idadi Kubwa ya walimu hawakuendelea na mchakato.
2\. Ratiba ya kufanya usahili wa kuandika hasa Kwa wenye masomo mawili. Mfano mtu aliekuwa na Historia zlikua anasubili mda mrefu kuja kufanya somo la pili hivo ngarama za kuishi zinaongezeka hasa Kwa wale wanaotoka mbali na eneo la usahili.
3\. Matumizi ya Technology ni madogo Katika uendeshaji wa usahili hivo kuongeza gharama Kwa wasahiliwa na serikali pia. Pia tunatumia muda mwingi Katika usahili Kwa kutotumia technology.
*Changamoto Kwa walimu (wasahiliwa)*
1\. Walimu wengi tumekata tamaa kitu ambacho ni kibaya. Kuitaka serikali ituajili walimu wote ni muujiza ambao hauwezi kutimi. Kukata tamaa kunafanya tukatae kira mchakato bali tunataka ajira. Mfumo wa zamani tumeupigia kelele na wasasa tunaupigia kelele je tunataka upi?
2\. Swala la changamoto za Majina kwene vyeti na vitambulisho. Hili Jambo wengi tumeshuhudia wasahiliwa wenzetu wakiondolewa kwenye mchakato bila huruma. Nini cha kufanya secretariat waliweka wazi nini cha kufanya mfano affidavit, Deadpool, barua ya utambulisho Kwa wale ambao hawana vitambulisho vinavyotakiwa lakini wengi hawakufanya hivo. Hivo vitu vipo na vinatolewa mda wote so kipindi cha usahili pekee. Hivo jiandae mapema. Pia tuwafundishe watoto na jamii Majina ni matatu ya ieleweke lipi la kati na la Mwisho.
Ukitaka kujua Kuna shida kamata mwanafunzi wa drs la 3 au 4 muulize ukoo wake nan? Utaskia majibu.
3\. Hatujiandai na usahili. Baadhi ya wasahiliwa hawachukui muda hata kujiandaa na vitu vidogo ambavyo vimeonekana kuhitajika kwene usahili. Nipo platform ambazo walimu tumeunganishwa tunakumbushana vitu, mfano groups za WhatsApp na telegram Kama ajiracoach inakusanya walimu nchi nzima.
*Maoni na mapendekezo*
1\. Mfumo wa kutumia usahili umeonekana kuwa bora kuliko ule wa zamani kwani angalau umekua shirikishi Kwa wasahiliwa hivo huko wazi ndiomaana imekua rahisi kubainisha hata changamoto. Hivo uboreshwe
2\. Nafasi za Kazi ziongezwe kwani zilizotolewa ni chache kulinganisha na walimu waliopo mtaani na uhalisia wa mahitaji shuleni.
3\. Idadi ya kuwa shortlisted ipungue au iendane na idadi ya nafasi ili kuwapunguzia Watu wengi zaidi mzigo ambao unajua hauwahitaji.
4\. Serikali iendelee kukasimisha madaraka hadi ngazi za wilaya ili kusogeza huduma zaidi Kwa walengwa.
5\. Usahili ufanyike kwa masomo zaidi ya moja Kwa siku. Hivo kuwe na siku maalumu ya kukagua vyeti na siku inayofuata ifanyike written interview.
6\. Nashauri walimu tuachane na hoja ya mwaka wa kumaliza chuo. Kila mtu ana haki ya kupata ajira Kwa ubora atakaouonyesha kwene enterview.
7\. Upimaji uongezeke Kwa kuuliza pia maswali ya content za somo husika na sio kua based kwene psychology na Curriculum pekee. Mfano mtihani uwe na maswali 50 Yan 25 misingi ya ualimu na 25 content za somo husika.
8\. Kuwepo na passmark inayotambulika Kama ni 50 au 80. Hivo kuwe na kanzidata maalumu Kwa watakaofanya vizuri kwene written na kushindwa kuchaguliwa kwenda oral kulingana na idadi. Hivo awamu nyingine watachukuliwa hao Kwanza na kwenda moja Kwa Moja kwenye oral enterview.
9\. Serikali itusamehe madeni yetu huko HSLB.
10\. Serikali kupitia halmashauri iandae Mpango maalumu Kwa kutupatia graduate mikopo yenye riba nafuu ili kujikwamua na kujiajiri. Kama wanakopoeshwa wasanii sisi tuna kosa gani?
Hiyo mikopo itasaidia pia kupunguza huu msuguano wa ajira chache kwani wengine watanyanyuka kiuchumi.
11\. Serikali isitishe udahili wa kozi ya ualimu vyuoni. Mfano DUCE, MUCE NA BUTIMBA TTC vifanywe kuwa vituo vya elimu mkondo wa amali ngazi za juu au hata VETA kabisa.
Kama sio hivo basi serikali itangaze rasmi kuakuanzia Mwakani ukiopt kusoma ualimu soma at your own risk serikali haitokuajiri Kwa muda unaotaka hivo mtu anaenda akijua.
Tuzingatie Ile principal ya *demands and supply na scale of preferences.*
*Mwisho.*
Karne hii ya 21 mtumo mzuri wa kupata watumishi ni serikalini na hata secta binafsi kuwashindanisha katika mfumo ambao ni wazi na shirikishi kwani hii inaongeza uharali Kwa wasahiliwa na serikali kuliko mfumo wa zamani ambao hujui Kwanini hukuchaguliwa. Pia serikali itoe Mrejesho Kwa wanaobahatika kufanya oral interview na hawajapangiwa vituo ili kujua Kama wamo kwenye kanzidata au wajipange upya hii italeta *peace of mind.*
*Naitwa MZINGA*
👍
👎
🖕
👏
😀
😮
🙏
🤣
12