
Samson Ernest
February 20, 2025 at 10:43 AM
UKIMTUMAINI MUNGU HUWEZI KUJUTA KATIKA MAISHA YAKO
Zab 84:12 SUV
[12] Ee BWANA wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.
Ukimtumaini mwanadamu unaweza kuambulia maumivu na machozi mengi katika maisha yako.
Unaweza kuweka matumaini kwa mtoto wako kuwa ataweza kukulea vizuri, badala yake akawa mtu hatari kwako.
Unaweza kuweka matumaini kwa mzazi wako atakufanyia kila kitu, ikatokea mzazi wako hayupo Duniani.
Unaweza kuweka matumaini makubwa kwa marafiki zako, mwisho wa siku wakageuka kuwa maadui zako wakubwa.
Unaweza kutumaini mali zako, utajiri ulionao ukaona ndio kila kitu kwako, chochote unaweza kufanya kupitia fedha ulizonazo. Ikafika wakati ukapata shida ambayo pesa inashindwa kuitatua.
Matumaini kwa watu na kwa vitu yanaweza kutufaa kwa muda mfupi Sana, baadaye yakatuacha kwa maumivu makali katika maisha yetu.
Tunapaswa kufahamu na kuweka akilini kuwa msaada wetu upo kwa BWANA, kufahamu hilo tunapaswa kumtumaini Mungu siku zote za maisha yetu.
Ukitaka kujilaumu na kuchukia watu bila sababu, na mpaka kukupelekea kumlaumu Mungu, weka matumaini yako kwa wanadamu, uwe na uhakika utaumia tu.
Hupaswi kusubiri yakupate mabaya, mtumaini Mungu siku zote za maisha yako, utaishi maisha ya ushindi siku zote hapa Duniani.
Mwisho, nikukaribishe kwenye channel ya wasap kupata maarifa mbalimbali kama haya, bonyeza link hii kujiunga=>>https://whatsapp.com/channel/0029VaD4A1c3WHTbZhfRBV3j
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
👍
❤️
😂
4