
Samson Ernest
288 subscribers
About Samson Ernest
Ninakualika katika kundi la kusoma biblia kila siku na kutafakari, kundi hili linaweza kuleta mabadiliko makubwa sana katika maisha yako. Utakutana na watu mbalimbali wanaosoma na kutafakari neno la Mungu kila siku. Watakuwa sababu ya kukufanya ukumbuke kusoma biblia kila siku. Wasiliana nasi kwa wasap namba +255759808081 ili uweze kuunganishwa kwenye group hili zuri la kusoma na kutafakari neno la Mungu. Soma neno ukue kiroho Liwe jua iwe mvua soma biblia yako Chapeo Ya Wokovu www.chapeo.or.tz +255759808081
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

MTU ANAYEFANYA UOVU KWA MTU ALIYEMTENDEA MEMA AWE NA UHAKIKA AMEKARIBISHA MATATIZO NA MABAYA YOTE Mit 17:13 SUV [13] Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, Mabaya hayataondoka nyumbani mwake. Siku za leo sio ajabu kumkuta mtu ambaye alitendewa mema mengi na mtu mwingine, mtu yuleyule alitetendewa mema akageuka na kumfanyia mabaya yule aliyemtendea mema. Tunaweza kuchukulia kawaida na kuona jambo hili ni la kawaida, ila ukweli lina matokeo mabaya sana kiroho na kimwili. Mtu anayerudisha mabaya kwa wale waliomtendea mema, awe na uhakika atavuna matatizo na mabaya mengi katika maisha yake. Mwanzo anaweza asione madhara ya ubaya wake, ila una matokeo ya kushangaza kwa mwenye ubaya huo, atapata shida ambayo anaweza akatafuta suluhisho lake asilipate haraka. Onyo hili la biblia linaweza kupuuzwa na msomaji asiyetafakari mambo kwa kina, ila mtu anayesoma kwa umakini na kutafakari, hatachukulia kawaida onyo hili. Tuwe makini katika maisha yetu, kuna watu hawakustahili kurejeshewa mabaya, wapo watu wamejitoa sana kwetu, wametufanya tufike hapo tulipofika, hawatastahili kulipwa mabaya. Tutende haki, tusimwonee mtu yeyote katika maisha yetu, wale waliotumiwa na Mungu kutufanya tufike mahali tumefika, tuhakikishe tunawapa heshima yao, na tujiepushe kuwatendea mabaya. Soma neno ukue kiroho Liwe jua iwe mvua soma Biblia na kutafakari Mungu akubariki sana Samson Ernest

Upekee wa Mwanamke... https://youtu.be/-BB6wkO9PKc?si=OIIQUsmJWJInmc4x

Faida za kuwa single...https://youtu.be/OXgLxPM1fvo?si=ABr18cHASIDDPBLp

KIBURI KINATANGULIA KABLA YA ANGUKO BAYA LA MTU Mit 18:12 SUV [12] Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu. Sio ajabu kuona mtu aliyefika viwango fulani vya utumishi wake akashuka chini ghafla, yale matendo makuu ya Mungu yaliyokuwa yanajidhihirisha kupitia yeye katika huduma yanakuwa hayaonekani tena. Bora usione matendo makuu ya Mungu kwa muda alafu huyo mtu awe salama kiroho, shida inakuja mtu huyo anapoteana kabisa, kile alichokuwa anakifanya na Mungu anaonekana kinakuwa hakionekani tena. Nini hutokea? Mtu anapofanya jambo la ki-Mungu, matendo makuu ya ki-Mungu yakadhihirika kwa uwazi, wengi huinuka na kuchukua utukufu wa Mungu. Huanza kujiona ni bora kuliko wengine, kile amekifanya na Mungu akaonekana kwa uwazi, badala ya kumtukuza Yesu na kumrudishia utukufu wake, wao hubeba hayo na kujiona wao ndio wamefanya kwa nguvu zao. Ukimsikiliza mtu aliyeinuka kiburi utamwona, vile anaongea anaonyesha wazi yeye ndiye anasababisha hayo mambo makuu ya Mungu yatokee kwa uwezo wao, na mara nyingi huondoa nafasi ya Mungu katika hayo. Ukiona kiburi kimekuwa kikubwa, ujue anguko lipo karibu mno, njia mojawapo ya anguko la mtu ni kiburi kuinuka ndani yake. Yak 4:6 SUV [6] Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. Ukimwona mwamini yeyote ameinuka kiburi au anaanza kuwa na kiburi mwombee haraka, au mshauri kwa upendo, kwa sababu anguko lake lipo karibu mno, kwa lugha rahisi kushuka kwake chini kupo mlangoni. Ukiona matendo makuu yanatokea kupitia huduma unayofanya, ongeza unyenyekevu mkubwa kwa Mungu, usije ukainua mabega, utashuka mshuko ambao kunyanyuka tena inaweza ikawa historia. Mtu mnyenyekevu ataendelea kula mema ya nchi, Mungu ataendelea kumtumia zaidi, sivyo hivyo tu, ataendelea kuongezeka viwango vya juu zaidi siku kwa siku. Ukitaka kuinuliwa juu na Mungu kwenye eneo lolote lile alilokupa Mungu utumike, liwe la kiroho au kimwili, kuwa mnyenyekevu sana kwa kila hatua unayopiga. Hata kama sasa unaonekana upo chini, kuwa na bidii sana na matokeo mazuri unayopata yasikupe kiburi, endelea kunyenyekea. Luka 14:11 BHN [11] Kwa maana yeyote anayejikweza atashushwa na anayejishusha, atakwezwa.” Maanguko mengi ya watu yanatokana na viburi vyao, wanaweza kukubali au kukataa ila kabla ya kuanguka kiburi kilitangulia, Mungu alivyo mwema aliwaonya kabla ya kuanguka kwao. Jilinde sana na kiburi, ni moja ya sumu mbaya sana kwa maendeleo mazuri ya mwamini, anaweza asifike hatima njema aliyoiweka Mungu katika maisha yake. Na mbolea nzuri ya kustawisha hatua zako ni unyenyekevu. Soma neno ukue kiroho Liwe jua iwe mvua soma Biblia na kutafakari Mungu akubariki sana Samson Ernest

*UKIELEWA HAYA NA KUTENDEA KAZI KWA VITENDO UTAINGIA KWENYE NDOA YA NDOTO YAKO* 🔹Soma sana vitabu mbalimbali vya kukujenga Kiroho na kimwili 🔹Soma sana biblia na kutafakari siku zote 🔹Omba sana Mungu bila kujalisha mazingira uliopo, tumia namna yeyote Ile kusema na Mungu wako. 🔹 Sikiliza mafundisho ya neno la Mungu huko YouTube, na mitandao mingine uliopo. 🔹Hudhuria semina za Neno la Mungu kadri uwezavyo, lengo lako likiwa kujaza maarifa sahihi. 🔹Jipende Sana, hii haimanishi usimpende Mungu, namaanisha usijidharau na kujiona hufai. 🔹Vunja mahusiano yote ya kingono na wanaume/wanawake unaotembea nao bila utaratibu. 🔹Vaa vizuri kutokana na uwezo wako, kuvaa vizuri sio lazima uvae nguo za ghali, unaweza kuvaa nguo ya mtumba ya 2,000 na ukapendeza. Ni ufahamu wako wa kuchagua na kupangilia vizuri rangi zinazoendana na wewe. 🔹Usione changamoto zinazokutokea kwenye maisha yako ni laana ya mababu na mabibi inakuandama, kumbuka wewe umeokoka. 🔹Kataa marafiki walioshindwa kwenye mahusiano, marafiki wenye mtazamo mbaya kuhusu wanaume na wanawake. 🔹Kuwa mtu wa ibada, kazi, chochote kinachopita kwenye mikono yako kifanye kwa ubora wa hali ya juu. 🔹Amini mume/ mke wako yupo na siku ukikutana naye utamtambua haraka kwa sababu umejaa maarifa mengi na maombi. 🔹Acha kufikiri mambo mabaya yaliyopita, Yale maisha uliyoishi na kukuharibu, kama umeshaachana na hayo maisha, usiendelee kuumia na kujilaani. 🔹 Usiogope kuachana na mtu ambaye unaona hamtawezana na moyoni mwako umekosa amani naye kutokana na tabia zake chafu zisizobadilika. 🔹 Usisahau kuwa Yesu anakupenda Sana, na alikufa kwa ajili yako. Hapendi kukuona ukipotea kuoa/kuolewa na mtu asiyefaa. Kaa katika haya utaona matokeo mazuri katika maisha yako, na utampata mwenzi wako sahihi. Soma Neno Ukue Kiroho Liwe Jua Iwe Mvua soma biblia Mungu akubariki sana Samson Ernest

*kupinga ukatili ni jukumu letu sote* https://youtu.be/fgYY8jg-_fY?si=PTmrMzuagJNl5Vu7

https://www.jamiiforums.com/threads/mambo-6-yanayomfanya-mwenye-haki-kustawi-katika-maisha-yake.2311833/#post-52982229

Thread 'Njia 5 zinazotumiwa na Mungu kumtegemeza mtu anapoteleza/kuanguka' https://www.jamiiforums.com/threads/njia-5-zinazotumiwa-na-mungu-kumtegemeza-mtu-anapoteleza-kuanguka.2312515/

YESU HAJAONDOKA NA AMANI YAKO || SAMSON ERNEST...https://youtu.be/YPYneM44wdM