
Samson Ernest
February 22, 2025 at 06:02 AM
*UKIELEWA HAYA NA KUTENDEA KAZI KWA VITENDO UTAINGIA KWENYE NDOA YA NDOTO YAKO*
🔹Soma sana vitabu mbalimbali vya kukujenga Kiroho na kimwili
🔹Soma sana biblia na kutafakari siku zote
🔹Omba sana Mungu bila kujalisha mazingira uliopo, tumia namna yeyote Ile kusema na Mungu wako.
🔹 Sikiliza mafundisho ya neno la Mungu huko YouTube, na mitandao mingine uliopo.
🔹Hudhuria semina za Neno la Mungu kadri uwezavyo, lengo lako likiwa kujaza maarifa sahihi.
🔹Jipende Sana, hii haimanishi usimpende Mungu, namaanisha usijidharau na kujiona hufai.
🔹Vunja mahusiano yote ya kingono na wanaume/wanawake unaotembea nao bila utaratibu.
🔹Vaa vizuri kutokana na uwezo wako, kuvaa vizuri sio lazima uvae nguo za ghali, unaweza kuvaa nguo ya mtumba ya 2,000 na ukapendeza. Ni ufahamu wako wa kuchagua na kupangilia vizuri rangi zinazoendana na wewe.
🔹Usione changamoto zinazokutokea kwenye maisha yako ni laana ya mababu na mabibi inakuandama, kumbuka wewe umeokoka.
🔹Kataa marafiki walioshindwa kwenye mahusiano, marafiki wenye mtazamo mbaya kuhusu wanaume na wanawake.
🔹Kuwa mtu wa ibada, kazi, chochote kinachopita kwenye mikono yako kifanye kwa ubora wa hali ya juu.
🔹Amini mume/ mke wako yupo na siku ukikutana naye utamtambua haraka kwa sababu umejaa maarifa mengi na maombi.
🔹Acha kufikiri mambo mabaya yaliyopita, Yale maisha uliyoishi na kukuharibu, kama umeshaachana na hayo maisha, usiendelee kuumia na kujilaani.
🔹 Usiogope kuachana na mtu ambaye unaona hamtawezana na moyoni mwako umekosa amani naye kutokana na tabia zake chafu zisizobadilika.
🔹 Usisahau kuwa Yesu anakupenda Sana, na alikufa kwa ajili yako. Hapendi kukuona ukipotea kuoa/kuolewa na mtu asiyefaa.
Kaa katika haya utaona matokeo mazuri katika maisha yako, na utampata mwenzi wako sahihi.
Soma Neno Ukue Kiroho
Liwe Jua Iwe Mvua soma biblia
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
🙏
2