
Christopher Peter
February 28, 2025 at 06:54 PM
Nimepata fursa adhimu ya kushiriki katika mapitio ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto katika mikoa ya Mwanza, Katavi, na Iringa. Lengo kuu la programu hii ni kuwaleta pamoja wadau kutoka sekta mbalimbali ili kushughulikia kwa pamoja masuala ya malezi, makuzi, na maendeleo ya awali ya mtoto.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Tanzania ina watoto zaidi ya milioni 16 wenye umri wa miaka 0 hadi 8, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuliko idadi ya watu katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki. Hii inadhihirisha kuwa kundi hili linahitaji uwekezaji mkubwa katika huduma za malezi, makuzi, na maendeleo ya awali ili kuhakikisha wanapata msingi imara wa maisha.
Zaidi ya asilimia 80 ya ukuaji wa ubongo hutokea katika kipindi hiki, hivyo ni wakati muhimu wa kuweka misingi sahihi ya afya, lishe, elimu, na ulinzi wa mtoto. Ushirikiano wa wadau wote ni msingi wa kuhakikisha watoto wanalelewa katika ma, soma zaidi https://www.facebook.com/share/p/15ig35
👍
🙏
2