
Christopher Peter - #MtotoNiMalezi
119 subscribers
Verified ChannelAbout Christopher Peter - #MtotoNiMalezi
Kuwekeza kwa watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 8 husaidia kujenga msingi imara wa ujuzi, afya, na tabia nzuri. Hii inachangia maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla kwa kukuza kizazi kinachoweza kuleta mabadiliko na kustawi kiuchumi.
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

DKT. BITEKO AWATAKA WAZAZI KUTUNZA FAMILIA ZAO “ Mtoto ni zao la matokeo ya wazazi wawili, Naomba wazazi tuthamini kuwa mtoto ni mtu muhimu na anahitaji kulelewa, tukumbuke kuwa tumefika hapa kwa kuwa wako wazazi walivumiliana na wakatulea katika familia na sisi tusiwe watu wa kutelekeza familia zetu, ni wajibu wa kila mmoja kujua kuwa familia ni msingi, tukijua kuwa kila mtu ana mapungufu hivyo tuvumiliane tulee familia zetu, ” Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Mei 24, 2025 jijini Mwanza wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia. #MaleziSummit #TMS2025 #MtotoNiMalezi

Tanzania Malezi Summit | 23–24 Mei 2025 Kauli mbiu: Uwekeza kwa Watoto Wetu! Kongamano hili limewakutanisha wadau na wataalamu kutoka sekta mbalimbali kujadili, kushirikishana uzoefu, na kuhamasisha uwekezaji katika malezi, makuzi, na maendeleo ya awali ya watoto. Miaka ya awali ndiyo msingi wa mafanikio ya baadaye! > “Asilimia 90 ya ukuaji wa ubongo hutokea kabla ya mtoto kufikisha umri wa miaka 8.” “Uwekezaji katika miaka 0–8 ni uwekezaji wenye tija zaidi kwa kizazi chenye uwezo wa kujifunza, kustawi na kuchangia maendeleo ya taifa.” Tukiwa pamoja – serikali, mashirika ya kiraia, sekta binafsi, wanazuoni, na jamii – tunaweka msingi thabiti kwa kizazi cha leo na kesho. Watoto wa leo, Taifa la kesho! #TanzaniaMaleziSummit2025 #UwekezaKwaWatotoWetu #Miaka0Hadi8 #MtotoKwanza #MtotoNiMalezi


#MtotoNiMalezi Mzazi au Mlezi ndiye mwalimu namba moja wa mtoto wake na kwa kiasi kikubwa sana mtoto hujifunza na kuiga mambo mbalimbali kutoka kwa mzazi au mlezi wake. 📌 Utafiti wa UNICEF (2021) unaonesha watoto huanza kutumia vifaa vya kidijitali kuanzia umri wa miaka 2–3. Huu ni wakati wa kuweka msingi wa matumizi salama ya teknolojia. KUMBUKA! Kipindi cha chini ya umri wa miaka 8 ukuaji na ujifunzaji wa maisha ya binadamu huchukua nafasi kubwa zaidi inakadiriwa zaidi ya 80% ya ukuaji wa ubongo hutokea wakati huo. Hii ni fursa pekee ya kujenga msingi wa maisha ya mtoto. Hivyo, Wazazi/walezi tuna nafasi ya kujenga kesho iliyojema kwa watoto wetu. Mambo Muhimu ya Kufanya: ✅ Zungumza na mtoto kuhusu hatari na fursa za mtandao. ✅ Weka muda na aina ya maudhui anayoweza kufikia. ✅ Tumia vifaa vya ulinzi (parental controls). ✅ Kuwa mfano wa matumizi salama na yenye maadili. Mtoto akilindwa vizuri mtandaoni, anakuwa huru kujifunza, kuchunguza na kukuza maarifa kwa usalama. #MaleziCampaing #Mtotokwanza


Tanzania Malezi Summit 2025 Mbele ya Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Doto Biteko, nilipata heshima ya kuwasilisha maendeleo na shughuli za TECDEN katika kuimarisha ushirikiano na kuratibu asasi zisizo za kiraia zinazojihusisha na malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto. ....."Hata sisi tumejengwa kwenye umri huo..." Nilisisitiza sababu za msingi kwa nini ni muhimu kuwekeza katika watoto chini ya miaka 8 — kipindi ambacho ubongo wa mtoto unakua kwa kasi zaidi kuliko kipindi kingine chochote maishani. Takwimu Muhimu: Tanzania ina takriban watoto milioni 16.1 (Sensa 2022) chini ya umri wa miaka 8, wote wakihitaji malezi bora na huduma za msingi za afya, lishe, na elimu. Takriban 30% (TDHS2022) ya watoto chini ya miaka 5 wanakabiliwa na tatizo la utapiamlo, jambo linalosababisha ucheleweshwaji mkubwa wa ukuaji wa ubongo na mwili. Utafiti unaonyesha kuwa ubongo wa mtoto hukua kwa 90% kabla ya kufikia umri wa miaka 8, na malezi bora pamoja na lishe bora huamua uwezo wake wa kujifunza, kuamua, na kuishi maisha yenye mafanikio. Kwa mujibu wa utafiti wa Afya ya uzazi wa mama na mtoto, asilimia 53 (TDHS2022) ya watoto wenye umri wa miezi 24 hadi 59 hawako kwenye mwelekeo sahihi wa ukuaji wa kawaida na kufikia ukuaji timilifu. Ushiriki wa wazazi, jamii, serikali, na wadau wote ni msingi wa kuhakikisha watoto hawa wanapata mazingira salama, yenye upendo, na yenye kuhamasisha ukuaji mzuri wa akili, mwili, na hisia. "Mtoto aliyepewa lishe bora, malezi chanya na elimu ya awali, Afya bora anakua na msingi thabiti wa maisha bora na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii." Tunaposhindwa kuwekeza sasa, tunapoteza fursa ya kuwa na kizazi chenye afya, wenye akili timamu, na wenye ufanisi katika maendeleo ya taifa letu. Tanzania inahitaji jitihada za dhati za kuhakikisha malezi bora kwa watoto wetu chini ya miaka 8, kama msingi wa taifa lenye nguvu, lenye afya, na lenye maendeleo endelevu. "Mtoto Ni Malezi: Msingi wa Familia Bora kwa Taifa Imara" #TanzaniaMaleziSummit2025 #Mtotonimalezi


Kila Mtoto Ana Mahitaji Yake! Huduma jumuishi ni njia ya kujenga fursa sawa kwa wote — bila kumwacha mtoto nyuma. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, takribani asilimia 49 ya Watanzania ni watoto chini ya miaka 18 — jambo linaloonyesha wazi kuwa mustakabali wa Taifa letu uko mikononi mwao. #MtotoNiMalezi #HudumaJumuishi #FursaSawaKwaWatoto

Uwekezaji katika umri wa miaka 0 hadi 8 ni msingi wa maendeleo ya binadamu na uchumi wa taifa. Tafiti za sayansi ya ubongo zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya ukuaji wa ubongo hutokea katika kipindi hiki, ambapo ubora wa lishe, afya, malezi, na ujifunzaji wa awali huathiri uwezo wa kognitivia, kihemko, na kijamii wa mtoto. Mazingira duni katika hatua hii yanaweza kusababisha athari zisizorekebishika, ikiwa ni pamoja na ukuaji duni wa ubongo na matokeo mabaya ya kiafya na kielimu. Utafiti wa Heckman (2006) unaonyesha kuwa kila dola moja inayowekezwa katika maendeleo ya awali ya mtoto inaweza kuzalisha faida ya hadi dola 13 kwa jamii kupitia ongezeko la tija na kupungua kwa gharama za afya na urekebishaji wa tabia. Kwa hivyo, uwekezaji katika utunzaji wa afya ya uzazi, lishe bora, elimu ya awali, na ulinzi wa mtoto unahakikisha kizazi chenye afya, uwezo wa kujifunza, na tija kwa uchumi wa taifa. #Agenda ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto

#Agenda ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Kikao cha mapitio ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Mkoa wa Mwanza #MaleziCampaing #Mtotokwanza #Tanzania

Nimepata fursa adhimu ya kushiriki katika mapitio ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto katika mikoa ya Mwanza, Katavi, na Iringa. Lengo kuu la programu hii ni kuwaleta pamoja wadau kutoka sekta mbalimbali ili kushughulikia kwa pamoja masuala ya malezi, makuzi, na maendeleo ya awali ya mtoto. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Tanzania ina watoto zaidi ya milioni 16 wenye umri wa miaka 0 hadi 8, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuliko idadi ya watu katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki. Hii inadhihirisha kuwa kundi hili linahitaji uwekezaji mkubwa katika huduma za malezi, makuzi, na maendeleo ya awali ili kuhakikisha wanapata msingi imara wa maisha. Zaidi ya asilimia 80 ya ukuaji wa ubongo hutokea katika kipindi hiki, hivyo ni wakati muhimu wa kuweka misingi sahihi ya afya, lishe, elimu, na ulinzi wa mtoto. Ushirikiano wa wadau wote ni msingi wa kuhakikisha watoto wanalelewa katika ma, soma zaidi https://www.facebook.com/share/p/15ig35