Salafi Da'wah East Africa
Salafi Da'wah East Africa
February 1, 2025 at 05:46 PM
............ *هؤلاء هم الرجال* *HAWA NDIO WANAUME.* *🌼 _'Affan bin Muslim Abu Uthman as-Swaffar (Allah Amrehemu)._* *_>>Alikusanya pamoja Ilmu na UchaMungu._* _>>Swalih bin Ahmad bin Abdillah al-I'jliy amesema:_ _"Ametuhadithia baba yangu:_ *_"'Affan bin Muslim ni mtu wa Basrah, thiqah, thabt, mtu wa Sunnah._* *Alipewa dinar elfu kumi ili asimuadilishe mtu fulani na wala asiseme-kuwa-:"Ni muadilifu wala-:sio muadilifu (katika Jarh na Taadil/Kujeruhi na Kuadilisha)."* *Basi akakataa na akasema:* *_"Wala sibatilishi haqi miongoni mwa haqi (nitabainisha hali yake kama ni muadilifu au sivyo)."_* _>>Hanbal bin Ishaq amesema:_ Nimemsikia 'Affan akisema: *"Aliniita Ishaq bin Ibrahim (alikuwa amiri wa mji wao chini ya khalifa Ma-muun) basi akanisomea barua ambayo alimuandikia al-Ma-muun ( aliyekuwa khalifa) na ndani yake yake-kumeandikwa-:* *_"Mtahini Affan (ili aseme kauli ya kufr na bida'h kuwa Quran imeumbwa) na muite ili aseme: "Qur'an ni kadhaa na kadhaa". Basi akisema hivyo mkubalie na mthibitishe juu ya jambo lake, na ikiwa hakukukubalia basi mkatie kile alichokuwa anapewa (kama mshahara/posho kutoka kwa mtawala)"_* na ilikuwa inamuendea yeye dirham mia tano kila mwezi. Amesema 'Affan: Basi akaniambia (yule Amiri): _"Unasemaje?"_ *Nikasoma:* {قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ} *_{{Sema: Yeye ni Allah Mmoja}}_* -(suratul-Ikhlas), hadi nikaihitimisha (sura hiyo). *Kisha nikasema: _"Imeumbwa hii (yaani hawezekani)?!"_* Basi akasema: _"Hakika Amirul-Mu'miniin anasema usipomuitikia (ukasema anavyotaka) anakata ulichokuwa unapewa (kama mshahara)."_ Basi nikasema;_*"Anasema Allah Taa'laa:*_ {وَفِى ٱلسَّمَآءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُون} *_{{Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa.}}_* *Basi akaninyamazia na nikajiondokea."* (ص228 - كتاب صفة الصفوة - عفان بن مسلم أبو عثمان الصفار - المكتبة الشاملة) *════ ❁✿❁ ════* *Salafi Da'wah East Africa (Afrika Mashariki)*
❤️ 3

Comments