
Salafi Da'wah East Africa
February 11, 2025 at 10:53 AM
*HUKMU YA KUFUNGA BAADA YA NUSU YA SHA'BAAN*
_"Ama kilichokuja kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم - kutoka kwa hadith ya Abu Hureira رضي الله عنه kuwa alisema: *(itakapofika nusu ya Sha'baan msifunge)* ameipokea Abu Daud na Tirmidhi._
_*Ulamaa wamekhtalifiana katika kuisahihisha na kuidhoofisha, wameidhoofisha wengi katika ulamaa wa hadith, kama Ahmad na ibn Ma'iin, na hata kwa kauli kuwa ni sahihi kama walivyoenda kwa kauli hiyo ibnul Qayyim na Al Albani, na ibn Baz -Allah awarehemu wote; linalokusudiwa ni katazo la kuanza kufunga baada ya nusu ya Sha'baan, ama aliyekuwa amefunga masiku mengi ya mwezi basi amepata Sunnah.*_
_Asema Sheikh Ibn Utheymiin رحمه الله تعالى -: *"na hata lau hadithi itasihi, basi katazo humo si ya kuharamisha, ni ya karaha (umakruhu) tu, kama walivyochukua kauli hiyo baadhi ya ahlul ilm, ila aliyekuwa na ada ya kufunga, basi atafunga hata baada ya nusu ya Sha'baan".*_
📗[Khutba: Ahkaamu shahri sha'baan; ya Sheikh Khalid Adh-dhafiry-Allah amhifadhi]
════ ❁✿❁ ════
*Salafi Da'wah East Africa (Salafi Da'wah Afrika Mashariki)*
https://whatsapp.com/channel/0029VabMSx07tkj3R6Dou41f
❤️
👍
5