Salafi Da'wah East Africa
February 22, 2025 at 10:40 AM
*TAHADHARI USIINGIE KATIKA MITEGO YA (POTE LA SHEITAN NA WASAIDIZI WAKE) KATIKA MWEZI WA RAMADHAN‼️*
*_Kama vile wenye kumtii Allah wanajiandaa kwa ajili ya mwezi huu, vile vile watu waovu wanajiandaa kwa ajili ya huu mwezi, lakini ni kujiandaa kishetani._*
*_Kwa hakika wengi wanajiandaa kufuatilia barnamij za channels na tv, na kufuatilia yanayopeperushwa, na matangazo ya ma-programu, ili achague yanayolingana naye katika mwezi huu, wallahul musta'an._*
*_Hakika pote la shetani na wasaidizi wake wamejitahidi katika miezi iliyopita; ili kuwaletea kazi zao katika mwezi huu, na mabaya yaliyoje waliyoyaandaa, wamewaandalia musalsalaat (series) za tabarruj na sufuur (wanawake kudhihirisha mapambo yao), na ikhtilaat (mchanganyiko ya wanaume na wanawake) na nyimbo;_*
*_Hili basi ni ikiwa katika hali zake nzuri, iweje ikiwa ni pamoja na kuipiga vita dini, na ubora, na kulifanya istihzai jambo la kushikamana na dini, na kulifanyia istihzai jambo la kuamrisha mema na kukataza maovu, na kuifanyia istihzai ilm ya kisheria na watu wake, na kuamsha sauti za kijahiliya (ukabila), na kulingania mambo twevu, na uovu na zinaa?!_*
*_Aliyepata hasara maskini ni anayevutwa na shetani na wasaidizi wake kuipoteza Ramadhan mbele ya (kuangalia/kufuatilia) munkar hizi zinazoangamiza, zinazowatia watu kwenye mtego kwa sababu mna ndani yake vichekesho na kuamsha shahwa, na mfano wa mitego kama hiyo._*
*_Au apoteze mtu wingi wa wakati wake katika mwezi huu; mwezi wa msamaha na rahma, kuangalia mpira/soka na michezo, ambayo yanapoteza mda bora, basi akajutia hilo siku ya Qiyamah._*
*_Basi ni vita vya kikweli, lakini ni vita vya kimaana iliyosalitishwa juu ya mioyo, wanabebwa kwayo wengi katika waislamu, na hawasalimiki ila wachache, basi tuzidhibiti nafsi zetu na tujiandae kwa siku ya Qiyamah, na tuihifadhi Ramadhan kutokamana na kila kinachochafua utahara wake na usafi wake, na kuipindisha kutoka kuwa ni mwezi wa kujitahidi juu ya twa'ah (kumtii Allah) hadi kuufanya ni mwezi wa ghafla na ma'siyah na kupoteza mda._*
📗[Khutba: Ramadhaanu aqbala ya baaghiyal kheir; ya Sheikh Khalid Ad-dhafiry-Allah amhifadhi]
════ ❁✿❁ ════
*Salafi Da'wah East Africa (Salafi Da'wah Afrika Mashariki)*
https://whatsapp.com/channel/0029VabMSx07tkj3R6Dou41f
❤️
🤝
👍
6