Salafi Da'wah East Africa
Salafi Da'wah East Africa
February 27, 2025 at 04:57 PM
*FUNGA NA FUNGUA NA WAISLAMU KATIKA NCHI ULIYOKO (1)* 1- IBN BAZ -ALLAH AMREHEMU. *_Ni juu ya muislamu kufunga na nchi aliyoko, na kufungua nayo, kwa kauli ya Mtume صلى الله عليه وسام: (funga ni siku mnayofunga, na fitr ni siku mnayofungua, na adh'haa ni siku mnayochinja) wabillaahi ttawfiiq._* 📙Chanzo: [Majmu' fatawa ibn Baz (15/102)] *_Linalodhihiri kwetu katika hukmu ya sheria takatifu ni kuwa la wajibu kwenu ni kufunga na waislamu walioko kwenu; kwa mambo mawili:_* _*Moja: kauli ya Mtume صلى الله عليه وسلم: (swaum ni siku mnayofunga na fitr ni siku mnayofungua na adh'haa ni siku mnayochinja) ameipokea Abu Daud na wengineo kwa isnad iliyo Hasan, basi wewe na ndugu zako mnapokuwa Pakistan ni mufunge wanapofunga na mufungue wanapofungua; kwa sababu mnaingia katika maongezi haya, na kwa sababu kuona mwezi kunakhtalifiana kwa kukhtalifiana matwali'.Na wameenda idadi ya ulamaa miongoni mwao ibn Abbaas رضي الله عنهما kuwa watu wa kila nchi wana muono wao*._ _*Jambo la pili: ni kuwa katika kuwakhalifu kwenu waislamu waliopo kwenu katika funga na kufungua mna kuleta tashwish na kuleta maswali na kuchukiana, na kuamsha mzozo na mihasama, na sheria ya kiislamu iliyokamili imekuja  kuhimiza juu kuafikiana na  kuja pamoja, na kusaidiana juu ya wema na taqwa, na kuacha mizozo na khilaaf; na kwa ajili hii asema Aliyetukuka: {Na shikamaneni na kamba ya Allah nyote na msigawanyike} na asema Mtume صلى الله عليه وسلم alipomtumiliza muadh na Abu Musa رضي الله عنهما  kuenda Yaman: (bashirini wala msikimbize/msifukuze na afikianeni wala mskhtalifiane)*_ 📙Chanzo: [Majmu' fatawa ibn Baz (15/103-104)] ════ ❁✿❁ ════ *Salafi Da'wah East Africa (Salafi Da'wah Afrika Mashariki)* https://whatsapp.com/channel/0029VabMSx07tkj3R6Dou41f
❤️ 👍 3

Comments