Salafi Da'wah East Africa
Salafi Da'wah East Africa
February 28, 2025 at 06:13 AM
*FUNGA NA FUNGUA NA WAISLAMU KATIKA NCHI ULIYOKO (3)* 3- AL-ALBANI -ALLAH AMREHEMU: *_Mimi naona wananchi wa kila nchi wafunge na nchi yao na asijitenge mtu; (eti) baadhi wanafunga nayo, na wengine wanafunga na nchi nyingine miongoni mwa waliotangulia katika kufunga au kuchelewa, kwa sababu mna katika hilo kupanua duara la ikhtilaaf baina ya watu wa nchi moja, kama ilivyotokea katika baadhi ya nchi za kiarabu, miaka kadhaa iliyopita. Wallaahul musta'an._* 📙Chanzo: [Tamaamul minnah- uk 398-399] Na alisema pia: _*Na tunaoona ni katika wajib kwa serikali za kiislam kufanya moja siku zao za kufunga na kufungua, kama wanavyofanya moja siku zao za hajj, laiti watawafikiana katika hilo. Kwa hiyo hatuoni raia wao wagawanyike, baadhi wafunge na nchi yao, na baadhi na nchi nyingine, na hilo ni katika mlango wa kuzuia mafsada makubwa kwa mafsada madogo kama ilivyo-muqarrar katika ilm ya usuul.*_ *_Wallaahu ta'ala waliyyu-ttawfiq._* 📙Chanzo: [As-silsilah As-Swahiihah - no. ya hadith 2624-254/6] ════ ❁✿❁ ════ *Salafi Da'wah East Africa (Salafi Da'wah Afrika Mashariki)* https://whatsapp.com/channel/0029VabMSx07tkj3R6Dou41f
❤️ 🎯 😁 5

Comments