SITTA SPORTS ARENA
SITTA SPORTS ARENA
February 9, 2025 at 12:12 PM
*CHASAMBI AOMBA RADHI⚽👇* *Napenda kuchukua fursa hii kuomba radhi kwa uongozi wa klabu, benchi la ufundi, wachezaji wenzangu, na zaidi ya yote, mashabiki na wapenzi wa Simba SC kutokana na makosa niliyofanya ambayo yamegharimu timu yetu.* *Najua jinsi mnavyoipenda na kuiunga mkono klabu hii kwa moyo wote, na ninaelewa kuwa matokeo yoyote yanayoiumiza timu pia huwaumiza ninyi kama familia yetu. Sikutamani kabisa kufanya kosa hilo, lakini ni sehemu ya mchezo, na najifunza kutokana na hali hii ili kuwa mchezaji bora zaidi kwa ajili yenu na timu.* *Naahidi kujituma zaidi, kujifunza kutoka kwa makosa yangu, na kurejea nikiwa na ari mpya ya kupigania mafanikio ya klabu yetu pendwa. Naomba radhi kwa yeyote aliyeumizwa na kitendo changu, na naomba muendelee kuniamini na kuniunga mkono.* SITTA SPORTS UPDATES ⚽

Comments