
SITTA SPORTS ARENA
106 subscribers
About SITTA SPORTS ARENA
*Sitta Sports Arena ni chaneli ya michezo inayojihusisha na Habari mbalimbali za michezo, matokeo pamoja uchambuzi. Pata Habari za michezo kuanzia za ndani na zile za kimataifa.* *Sitta Sports Arena Deals with All Sports Updates and Sports analyst also Highlights of Football Match and results*
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

*NICO ANUKIA BARCA⚽* Msimu uliopita klabu ya Barcelona ilikuwa timu tishio zaidi katika safu ya ushambuliaji, umahiri wa kinda Lamine Yamal, Raphinha na Robert Lewandowski ulitosha kabisa kuifanya Barca kuwa hatari, wapinzani wao wakuu katika ubingwa pale Hispania Real Madrid ni mashahidi kwa fedheha walizokumbana nazo msimu uliopita. Licha ya ubora huo Barcelona wanatajwa kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili winga wa Atletic Bilbao, Nico Williams. SITTA SPORTS UPDATES ⚽


*MAGAZETI YA MICHEZO LEO TAREHE 15/JUNI/2025⚽👇* SITTA SPORTS UPDATES ⚽

*SIMBA KURUDI KWA LAKRED TENA⚽* Klabu ya Simba SC inafikiria kumrudisha tena golikipa Ayoub Lakred kurudi kuitumikia klabu hiyo kuelekea msimu ujao. Viongozi wa Simba SC wanasubiri ripoti rasmi ya benchi lao la ufundi ikiwa litamuhitaji Ayoub Lakred watamrudisha kikosini. - SITTA SPORTS UPDATES ⚽


*GATTUSO KOCHA MPYA WA ITALIA⚽* Rasmi sasa Gennaro Gattuso ataingia kama kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Italia kuelekea Fainali za kombe la Dunia 2026. Makubaliano yamemalizika na Gattuso hivi karibuni atatangazwa kuwa Kocha wa Italia kuiendea misheni maalumu ya kurudisha heshima ya Italy kwenye Kombe la Dunia la 2026 SITTA SPORTS UPDATES ⚽


*KENGOLD KUWASILI KESHO TABORA ⚽* Wachezaji wa Kengold Fc 🇹🇿 wametumiwa nauli na Uongozi wa Klabu hiyo ili wafike Tabora kwaajili ya mechi ya NBC PL 🇹🇿 dhidi ya Simba Juni 18 ✅ Kila mchezaji atasafiri kivyake na wataanza kuwasili Tabora kesho Jumatatu kwaajili ya mechi ya Jumatano 👀 SITTA SPORTS UPDATES ⚽
