Nurul Kitab Wa Sunnah
Nurul Kitab Wa Sunnah
February 22, 2025 at 06:11 PM
*WAUME WAKO WENGI LAKINI WA NAMNA HII WACHACHE SANA USITHUBUTU KUMUUDHI.* *------•<°○●🕸●○°>•-------* 1. Mume ambaye anapoingia ndani ya nyumba yake, jambo la kwanza analouliza ni juu ya utekelezaji wa ibada ya swala na usomaji wa Qur'an kwa waliomo. Kuanzia mke, watoto na wengine. Huyo ndio Ana mapenzi ya kweli na Familia yake na lengo ni kwenda nao peponi. ewe mwanamke Usimbughudhi utakula hasara duniani na akhera. 2. Mume ambaye ana wivu na mke/wake wake. Na Alama ya wivu huo na kuhakikisha mke wake haonyeshi maumbo yake kwa wanaume wengine. Kwa hivyo humnunulia mke wake mavazi ya stara na hatoi ruhsa ya kutoka isipokuwa kajistiri kisheria. Kwani anajua kuwa kutokumsitiri mke vyema, nikukaribisha mihitihani kwa mke wake. Kwani hata waume wenzake nao wana matamanio. Na wala hakaribishi mazoea ya wanaume wengine kwa mke wake. Huyo ndio anakupenda na anajua maana kupenda. Na wala hayuko tayari kushare pendo Hilo na mwanaume mwingine. Mng'ang'anie wachache Hao. 3. Mume ambaye maamuzi ya familia yake hayako Katika mikono ya watu wengine. Sio kwa wazazi wala marafiki. Anasimamia mwenyewe maamuzi ya familia yake. Labda Katika jambo amabalo sheria imemtaka atake msaada kwingine. Huyo ndio mwanaume aliefahamu maana ya usimamizi wa familia. Dada yangu huyo ndio mume Hebu mkamatilie sana. 4. Mume ambaye anakuwa kama maji. Usipoyanywa utayaoga....... Kwa maana ni mwanaume mahiri na hodari Katika maisha ya kifamilia. Mkali panapohitaji ukali, laini sana panapohitaji ulaini. Penye ucheshi ndio usiseme. Kwa uhodari wake huwa unammisi hata anapoenda kazini sikwambii akisafiri. Mume mnyenyekevu hajui kunyanyua mkono wake kumpiga mke wake. Dada yangu Hao wachache mno. Mpende mno. 5. Mume mkarimu mwenye mapenzi na watoto, ndugu na jamaa zake na za mke wake, hana ubaguzi wa Aina yoyote Ile. furaha yake nikuona familia yake wanafuraha. Hutanguliza wanachokitaka kabla ya kile anachokitaka yeye madhali hakiendi kinyume na sheria za Muumba. Huyo ni Katika wanaume wenye sifa za kipekee. Wachache mno Kamatana nae. 6. Mume ambaye ambaye anakupa nafasi ya kujadili na kutoa mawazo yako Katika jambo. Anakusikiliza hata unaongea ujinga. Na hata kama hajakubaliana na ushauri huo. Basi hukupongeza kwa ushauri wako na kuusifia, Kisha hutoa maamuzi yake kwa busara ya hali ya juu. Kiasi cha wewe kuridhika na maamuzi yake. Huyo ni Katika wanaume wachache wenye kujua thamani ya mke. Usimkere ukaja kumpoteza. 7. Mume ambaye anakutanguliza Katika kila kitu sio kwenye chakula wala mavazi na mambo mengine, hali mpaka akakikishe umekula, havai mpaka akakikishe umevaa. Haijalishi kipato chake, anakuenzi kwa kiwango cha kipato chake. Raha yake aone unapendeza. Na kuwa na afya bora. Hakusimbulii kwa kile alichokupa. Ana maneno mazuri hata anapokuwa amekasirika. Maumivu yako ndio Maumivu yake. Upewe nini Dada yangu Hebu mpaka avimbiwe na mapenzi. 8. Mume ambaye akiingia ndani ya nyumba huukabidhi mwili wake na akili yake kwako umsanifu utakavyo. Akiwa anajua kuwa huo ni muda wako wa kutekeleza majukumu yako kwake. Wewe ndio TV yake wewe ndio Whatsapp yake. Ili kupatikane ile misingi matatu ya ndoa, utulivu, mapenzi na huruma. Dada ukimpoteza utajuta. Hiyo zawadi kutoka kwa Mola wako. 9. Mume ambaye pindi mnapotofautiana, ukimrejesha kwa Allah na Mtume wake (Qur'an na sunnah). Basi huwa mdogo sana. Mwepesi sana wa kuomba msamaha, anapokuwa kakosea hujishusha sana kwako. Sio mshindani hana gubu, hupenda kusikiliza, anapenda mjadala wa kheri Kati yenu. Dada yangu huyu ni Katika wachamungu. Ukizirusha shauri yako. Mpende mno. 10. Pamoja na mapenzi, kukuenzi, kukujalia vyote hivyo. Havina thamani kwake ikiwa utakuwa unachupa mipaka ya Allah aliyetukuka. Mapenzi yake kwa aliemuumba ni makubwa zaidi kukilo kwako. Ili akupende zaidi ni pale atakapompenda yule anaempenda zaidi. Na mnapotofautiana Katika haki ya Muumba na haki yake huwa hakurupuki kuchukua maamuzi kwa mujibu wa akili yake. Bali huangalia Qur'an na sunnah zimemuelekeza vipi. Ukisikia mwanaume wa peponi ndio huyo. Ni zawadi kwako huyo. Hakika ukomo wa furaha ya mwanamke hapa duniani ni kupata mume mwenye mapenzi ya dhati, heshima huruma na mwenye kujali. *Mume mwema ni ndoto ya kila mwanamke mwenye kujitambua ukimpata usimpoteze ni wachache mno* *------•<°○●🕸●○°>•-------*💦 *UKIYAPENDA YACHUKUE KAMA YALIVYO* https://whatsapp.com/channel/0029VavTCy51XquRQdoPOJ0t OA au OLEWA na Mtu sahihi Kwani NDOA NI TAMU ➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿
🌺 1

Comments