Nurul Kitab Wa Sunnah
Nurul Kitab Wa Sunnah
February 26, 2025 at 11:47 AM
*❗❗NDUGU ZANGU TUMCHE ALLAAH ﷻ* JAMBO LA TALAKA NI HALALI LAKINI LA MCHUKIZA ALLAAH ﷻ USIPENDE KUOA NA KUACHA *Wahurumieni Wanawake zenu Ndyo ALLAH ﷻ alicho tuhusia na Mtume ﷺ Kama Mwanaume Huna Huruma na Mke wako, Mtakua na Tofauti Gani❓❓Je,❓Hutambui kua Mkeo ni Dhaifu Wahitajia Kua na Kauli Njema Nasiyo kutoa talaka kama Vile Maji ya Kunywa, Jambo Hili la Chukiza Mnooo❗* ALLAH ﷻ anasema وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا *Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Allah ﷻ ametia kheri nyingi ndani yake.* [Surah An-Nisa' 19] Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: *katika Aayah nyingine ya sura hiyo hiyo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anaendelea kututanabaisha* وأخذن منكم ميثاقا غليظا *“…Nao wanawake wamepokea kwenu ahadi thabiti (kuwa mtakaa nao kwa uzuri).”* [An-Nisaa: 21] *Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akielezea fadhila za tabia njema anasema:* أكمل المؤمنين إيمانا أحسنهم خلقا, وخياركم خياركم لنسائهم خلقا *❝Muumini aliyekamilika kwa imani ni yule mwenye tabia njema, na mbora wenu ni yule aliye mbora kwa wake zake kwa tabia.❞* [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy] *Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema tena:* خيركم خيركم لأهله , وأنا خيركم لأهلي *❝Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani (ahli).❞* [Ibn Maajah na Ad-Daarimy] *Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:* إنّ المرأة خلقت من ضلع وإنّ أعوج شيئ في الضّلع أعلاه , فإن ذهبت تقيمه كسرته , وإن تركته لم يزل أعوج , فاستوصوا بالنساء *Mwanamke Ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na lau utauacha utaendelea kupinda, nakuusieni (kuwafanyia wema) wake zenu.”* [Al-Bukhaariy na Muslim] *Tuishi kama alivyo tuelekeza Mtume ﷺ na ALLAH ﷻ Mwanaume watakikana uwe na Subra na Uvumilivu usiwe kama Mkeo Mwanamke ni Mdhaifu Sana* *والله أعلم* ⚖════❁(🔘)❁════⚖ Mja dhalili kwa ALLAH ﷻ: *Abūl Qayyim al sa'adiyy-Allaah amhifadhi* Kwa faida zaidi Tembelea Channel yetu kupitia kiunganishi👇 WhatsApp Channel https://whatsapp.com/channel/0029VaZ971X2kNFh1Yng9447 Jiunge na Telegram👇👇 https://t.me/+q05hwRmp4uNiYzJk
❤️ 3

Comments