
GPSA TANZANIA
February 6, 2025 at 06:09 PM
GPSA YAFANYA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI 2025
Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) imefanya Mkutano wa tatu wa Baraza la sita la Wafanyakazi wa GPSA siku ya Jumanne tarehe 04/02/2025 katika ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa ya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Kikao cha Baraza kiliongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala Profesa Geraldine Arbogast Rasheli akisaidiana na Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Stephen Muro.
Mwenyekiti wa Baraza Prof. Rasheli aliongoza mjadala wa masuala mbalimbali ikiwemo randama ya bajeti ya Wakala 2025/26, Hoja za Wafanyakazi pamoja na masuala mengine yaliyojitokeza yanayohusu Wakala.
Prof. Rasheli alisisitiza watumishi kuongeza bidii katika utendaji kazi na kuwa wabunifu ili kuwezesha kuongeza mapato na kufikia malengo ya Wakala.
Prof. Rasheli alihitimisha kwa kuwapongeza na kuwashukuru watumishi wanaotarajia kustaafu Utumishi wa Umma hivi karibuni katika Wakala na kuwatakia maisha mema.
#gpsatanzania #boharikuuyaserikali
https://www.instagram.com/p/DFvFMPCtER-/?igsh=MW5vMWtvcThhbXk0cQ==