
Swautu Jamil Islamic Daawa
January 31, 2025 at 04:54 AM
*๐ HUKMU YA SWALA YA IJUMAA ๐*
Swala ya Ijumaa ni miongoni mwa swala muhimu za faradhi. Na ni wajib kwa kila Muislamu mwanamume ,mwenye akili timamu, alie baleghe ambae hana nyudhuru za kisheria za kumzuia kuetekeleza ibada hiyo.
Na sharia imetia mkazo zaidi na kusisitiza kutekelezwa swala ya ijumaa kwa jamaa. Na malipo yake ni makubwa zaidi.
*โก๏ธ. FADHLA ZA SIKU YA IJUMAA*
โ๏ธ. Kupata Thawabu na Malipo kwa kila hatua ya kwenda Msikitini sawa na Mtu aliyesimama kuswali na kufunga Mwaka mzima. Amesema Mtume ๏ทบ:
ู
ููู ุงุบูุชูุณููู ููููู
ู ุงููุฌูู
ูุนูุฉู ููุบูุณูููู ููุจููููุฑู ููุงุจูุชูููุฑู ููุฏูููุง ููุงุณูุชูู
ูุนู ููุฃูููุตูุชู ููุงูู ูููู ุจูููููู ุฎูุทูููุฉู ููุฎูุทููููุง ุฃูุฌูุฑู ุณูููุฉู ุตูููุงู
ูููุง ููููููุงู
ูููุง] ุฑูุงู ุงูุชุฑู
ุฐู ูุฃุญู
ุฏ]
[Mwenye kuoga na kujisafisha, kisha akaenda Msikitini na mapema na akamkurubia Khatibu na akasikiliza kwa utulivu. Mwenyezi Mungu ๏ทป atamlipa kwa kila hatua malipo sawa na Mtu aliyesimama kuswali na kufunga Mwaka mzima] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Ahmed].๐
โ๏ธ. Kusamehewa Madhambi yake ya wiki mzima pamoja na siku tatu za ziada. Amesema Mtume ๏ทบ:
ู
ููู ุชูููุถููุฃู ููุฃูุญูุณููู ุงููููุถููุกู ุซูู
ูู ุฃูุชูู ุงููุฌูู
ูุนูุฉู ููุงุณูุชูู
ูุนู ููุฃูููุตูุชู ุบูููุฑู ูููู ู
ูุง ุจููููููู ููุจููููู ุงููุฌูู
ูุนูุฉู ููุฒูููุงุฏูุฉู ุซูููุงุซูุฉู ุฃููููุงู
ู] ุฑูุงู ู
ุณูู
]
[Mwenye kutawadha vizuri, kisha akaja Msikitini na akamsikiliza Khatibu na kunyamaza. Anasemehewa Madhambi yake ya wiki mzima pamoja na siku tatu]. [Imepokewa na Muslim.] ๐
โ๏ธ. Kukubaliwa dua katika siku hii tukufu. Amesema ๏ทบ:
ููู ุงููุฌูู
ูุนูุฉู ุณูุงุนูุฉู ููุง ููููุงููููููุง ุนูุจูุฏู ู
ูุณูููู
ู ููุงุฆูู
ู ููุตููููู ููุณูุฃููู ุงูููููู ุฎูููุฑูุง ุฅููููุง ุฃูุนูุทูุงูู] ุฑูุงู ู
ุณูู
]
[ Hakika katika Siku ya Ijumaa kuna wakati, haafikiwi Muislamu na wakati huo hali akiwa anamuomba Allah Kheri, ila Mwenyezi Mungi humpatia]. [Imepokewa na Muslim] ๐
*โก๏ธ. ADABU NA SUNNA ZA SIKU YA IJUMAA*
1๏ธโฃ.Kuoga na kujisafisha na kupaka manukato mazuri pamoja na kuondosha harufu mbaya mwilini.. Amesema Mtume ๏ทบ:
ู
ููู ุงุบูุชูุณููู ููููู
ู ุงููุฌูู
ูุนูุฉู ุบูุณููู ุงููุฌูููุงุจูุฉู ุซูู
ูู ุฑูุงุญู ููููุฃููููู
ูุง ููุฑููุจู ุจูุฏูููุฉู] ุฑูุงู ุงูุจุฎุงุฑู ูู
ุณูู
]
[ Mwenye kuoga siku ya Ijumaa, Josho la Janaba kisha akaenda Msikitini (na mapema.) Mfano wake ni kama mtu aliyetowa sadaka ya Ngamia] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]๐
2๏ธโฃ. Kwenda Msikitini mapema na kumkurubia khatibu. Amesema Mtume ๏ทบ:
ุงุญูุถูุฑููุง ุงูุฐููููุฑู ุ ููุงุฏููููุง ู
ููู ุงููุฅูู
ูุงู
ู ] ุฑูุงู ุฃุจูุฏุงูุฏ]
[Nedeni mkasali sala ya Ijumaa, na mkae karibu na khatibu]. [Imepokewa na Abuu Daud]๐
3๏ธโฃ. Kujishughulisha kwa Kumtaja Allah, kusoma Qurโan, kuomba msamaha, kuomba dua kwa wingi na kumsalia Mtume Muhammad ๏ทบ.
4๏ธโฃ. Kumsilikiza Khatibu kwa utulivu, bila ya kujishughulisha na mambo mengine. Asema Mtume ๏ทบ:
ู
ููู ุชูููุถููุฃู ููุฃูุญูุณููู ุงููููุถููุกู ุซูู
ูู ุฃูุชูู ุงููุฌูู
ูุนูุฉู ููุงุณูุชูู
ูุนู ููุฃูููุตูุชู ุบูููุฑู ูููู ู
ูุง ุจููููููู ููุจููููู ุงููุฌูู
ูุนูุฉู ููุฒูููุงุฏูุฉู ุซูููุงุซูุฉู ุฃููููุงู
ู] ุฑูุงู ู
ุณูู
]
[Mwenye kutawadha vizuri, kisha akaja Msikitini na akamsikiliza Khatibu na kunyamaza. Anasemehewa Madhambi yake ya wiki mzima pamoja na siku tatu]. [Imepokewa na Muslim.] ๐
*โก๏ธ. MAMBO YALIO KATAZWA KATIKA SWALA YA IJUMAA*
1๏ธโฃ. Kuja Msikitini kuchelewa na kukata safu kwa kuruka watu, kwa lengo la kutaka kukaa safu ya mbele. Siku moja Mtume ๏ทบ alimuona mtu akikata safu na kuruka watu; Akamuambia:
ุงุฌูุณ ููุฏ ุขุฐูุช ูุขููุช] ุฑูุงู ุฅุจู ู
ุงุฌุฉ]
[Kaa chini kwa hakika umewaudhi watu na umechelewa.] [Imepokewa na Ibnu Maajah]
2๏ธโฃ. Kuwashawishi waja wa Mwenyezi Mungu, kwa kusoma Qurโan kwa sauti kubwa, au kufanya Dhikri kwa sauti ya juu. Mtume ๏ทบ aliwakataza Masahaba kusoma kwa sauti ya juu, na akawambia; Asisome mmoja wenu Quraโn kwa sauti ya juu kuliko mwingine.
3๏ธโฃ. Kuzungumza wakati wa Khatibu anatoa khutbah ya Ijumaa. Amesema Mtume ๏ทบ:
ู
ู ูุงู ูุตุงุญุจู ููู
ุงูุฌู
ุนุฉ ูุงูุฅู
ุงู
ูุฎุทุจ ุฃูุตุช ููุฏ ูุบุง] ุฑูุงู ุงููุณุงุฆู]
[Ukimuambia mwenzako nyamaza na Khatibu akiwa anazungumza, amefanya upuzi]. [Imepokewa na Al-Nnasaai] ๐
*โก๏ธ. KHATARI YA KUACHA SWALA YA UJUMAA*
Mtume Muhammad ๏ทบ Amesisitiza na kutilia mkazo juu la suala la kutekeleza swala ya Ijumaa. Na akawatahadharisha Waislamu wanaoacha kutekeleza swala hii. Adhabu kubwa watakayo pata watu hao hapa duniani ni nyoyo zao kuwa ngumu na kupigwa muhuri wa kughafilika. Amesema Mtume ๏ทบ:
ูููุชููู ุฃููุงู
ุนู ูุฏุนูู
ุงูุฌู
ุนุงุชุ ุฃู ููุฎุชู
ู ุงููู ุนูู ูููุจูู
ุ ุซู
ูููููู ู
ู ุงูุบุงูููู] ุฑูุงู ู
ุณูู
ูุฃุญู
ุฏ ูุงููุณุงุฆู]
[Hawataendelea watu kuacha swala ya Ijumaa, mpaka Mwenyezi Mungu apige muhuri nyoyo zao, kisha watakuwa niwenye kuishi katika mughafala]. [Imepokewa na Muslim na Ahmad na Al-Nnasaai]๐
Ndugu Muislamu, tujihadhari sana na kuacha swala ya Ijumaa, kwasababu adhabu yake ni nzito sana. Moyo ukiwa mgumu, basi mwanadamu anakuwa sawa na myama, hajali lolote wala chochote. Utamuona hamuogopi Mwenyezi Mungu, kwa kufanya maasi usiku na mchana.
Tunamuomba Allah Subhaanahu wa Taala athibitishe nyoyo zetu juu ya twaa yake, na atulinde na machafu yote.