
SamWaMiiracareTz
February 26, 2025 at 12:54 PM
*VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS)*
✍🏾Vidonda vya tumbo ni ugonjwa wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula katika mwili wa binadamu, ambapo kuta za mfumo wa uchakataji wa chakula huchubuka. Ni vidonda vinavyopatikana ndani ya mfumo wa tumbo. Ugonjwa huu huathiri zaidi watu wazima na kwa kiasi kidogo sana kwa watoto wadogo.
✍🏾Vidonda vya tumbo huweza kuwa;
-Ndani ya mfuko wa tumbo kuu la kuhifadhi chakula na vikiwa huko hufahamika kama *Gastric Ulcers*
-Sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba na huitwa *Duodenal Ulcers*
-Sehemu ya mwisho/chini ya koromeo la chakula na huitwa *Esophageal Ulcers*
✍🏾Vidonda vya tumbo husababishwa na; ❌Tindikali (Acid) inayopatikana ndani ya tumbo,
❌Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori) bacteria hawa huanza kushambulia baada ya kuta za tumbo kuchubuliwa na acid, ❌Kutokula chakula kwa wakati unaostahili, ❌Msongo mkali wa mawazo,
❌ Kula vyakula vyenye tindikali (acid) nyingi mara kwa mara,
❌Uvutaji wa sigara,
❌ matumizi ya vilevi vikali.
*✍🏾Viashiria vya kuwa kuna tatizo la vidonda ndani ya tumbo ni kama;*
👎🏾Kuwa na maumivu makali hasa baada ya kula,
👎🏾 Kuumwa tumbo baada ya kula vyakula kama dagaa, maharage na pilipili,
👎🏾 Kuumwa mgongo au kiuno,
👎🏾Kiungulia,
👎🏾Tumbo kujaa gesi na Kucheua mara kwa mara
👎🏾Kukosa hamu ya kula
👎🏾Tumbo kuwaka moto,
👎🏾 Kukosa choo au kupata choo kwa shida,
👎🏾Kichefuchefu au kutapika
👎🏾 Kushindwa kupumua vizuri
*✍🏾Tatizo la vidonda vya tumbo lisipotibiwa hupelekea;**
👉🏾Kupata haja kubwa iliyochanganyika na damu,
👉🏾Kuchoka bila sababu maalumu,
👉🏾Kupungua kwa nguvu za ki-ume,
👉🏾Kizunguzungu,
👉🏾Sehemu za mwili kupata ganzi,
👉🏾Kusahausahau na hasira bila sababu,
👉🏾 Kukosa hamu ya kula.
Vikishamiri sana huweza kusababisha athari zaidi.