KitaaCtics: Where the Elite Meets The Streets
KitaaCtics: Where the Elite Meets The Streets
February 11, 2025 at 05:33 PM
*Si Mbaya Kujua* Je, unafahamu kuwa kibwagizo kilichoimbwa na *Kelly Rowland* katika wimbo uliotamba sana mwanzoni mwa miaka ya 2000, *Dilemma* (akiimba na Nelly), haikuwa utunzi original? Basi kama hukujua leo nakusanua, kibwagizo kile ilikuwa ni cover ya sehemu ya wimbo wa *Patti LaBelle uitwao Love, Need and Want You,* ambao ulitoka mwaka 1983 katika albamu yake *I am in Love Again.* Cha kuvutia zaidi ni kwamba licha ya wimbo huo wa awali kuwa maarufu katika enzi zake, ulimwengu wa muziki ulishuhudia kizazi kipya kikiupokea wimbo wa Dilemma vizuri sana, bila hata kujua kuwa melody ya Kelly Rowland ilikuwa imechukuliwa moja kwa moja kutoka kwa diva mkongwe, Patti LaBelle. Kipande cha mwanzoni cha kibwagizo _”I love you, I need you Nelly, I love you, I do ”_ kinafanana kabisa na jinsi Patti LaBelle alivyoimba karibu miongo minne iliyopita! Mafanikio ya Dilemma yalikuwa makubwa mno, ikikaa kwenye nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 kwa wiki 10 mfululizo na kushinda tuzo ya Grammy. Wimbo huu ulibadilisha kabisa tasnia ya muziki wa R&B na hip-hop kwa kuchanganya vionjo vya zamani na vipya, huku ukiendelea kuwa wimbo ulioteka hisia za mashabiki wa mapenzi kote ulimwenguni. Cha kushangaza zaidi? Patti LaBelle mwenyewe alishangazwa na jinsi kizazi kipya kilivyopenda kibwagizo hicho, kiasi cha kujiunga na Kelly Rowland jukwaani mara kadhaa kuimba wimbo huo pamoja! Hii ni moja ya nyakati ya kudhihirisha nguvu ya muziki pale unapovutia, haijalishi ulitoka lini, utadumu milele! Upo? *Mjombaako* *©️BantuKwanza*
❤️ 2

Comments