KitaaCtics: Where the Elite Meets The Streets
KitaaCtics: Where the Elite Meets The Streets
February 15, 2025 at 11:49 AM
*SI MBAYA KUJUA* *GWIJI LA MUZIKI MWENYE KALAMU YA DHAHABU* Kama wewe ni mpenzi wa muziki wa R&B utakuwa umeshawahi kulisikia jina la *Kenneth ‘Babyface’ Edmonds*, mtunzi na mtayarishaji aliyebarikiwa kipaji cha kipekee katika uandishi wa nyimbo za R&B, Slow Jams, na New Jack Swing. Mguso wake wa kipekee umeacha alama isiyofutika katika mioyo ya wapenda muziki wengi, akiandika na kutengeneza nyimbo ambazo zimekuwa kilele cha hisia na kumbukumbu kwa vizazi mbalimbali. Ukizungumzia muziki wa mapenzi ule unaonata moyoni kama asali, wenye sauti zinazosoothen hisia kama upepo mwanana wa jioni basi jina la Babyface lazima litokee kwenye mazungumzo. Aliandika, alitayarisha, na mara nyingi alishiriki uimbaji wa nyimbo zilizotufanya tupendane, tuhuzunike, tukumbuke, na wakati mwingine tufikirie maisha kwa kina zaidi. Pale unaposikia End of the Road ya Boyz II Men na ghafla unahisi dunia inasimama kidogo, ama unapofumba macho ukisikiliza Breathe Again ya Toni Braxton na hisia zikawa nyingi kuliko maneno, yes huyo ni Babyface kwenye kazi yake. Yawezekana wewe ni mmoja wa watu ambao umesikiliza sana nyimbo ambazo mashairi yake jamaa huyu ndio alihusika kuyaandika bila wewe kujua. Leo ninakusanua na kukukuletea orodha ya nyimbo 40 maarufu sana ambazo Babyface ameshiriki katika uandishi wake, ikionyesha kipaji chake na mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki: 1. I’ll Make Love to You - Boyz II Men 2. End of the Road - Boyz II Men 3. Exhale (Shoop Shoop) - Whitney Houston 4. Breathe Again - Toni Braxton 5. Another Sad Love Song - Toni Braxton 6. Not Gonna Cry - Mary J. Blige 7. Take a Bow - Madonna 8. Superwoman - Karyn White 9. You are Making Me High - Toni Braxton 10. My, My, My - Johnny Gill 11. Can We Talk - Tevin Campbell 12. I Am Your Baby Tonight - Whitney Houston 13. Red Light Special - TLC 14. Ready or Not - After 7 15. Rock Steady - The Whispers 16. Roni - Bobby Brown 17. Don’t Be Cruel - Bobby Brown 18. Every Little Step - Bobby Brown 19. Baby-Baby-Baby - TLC 20. Change the World - Eric Clapton 21. Love Shoulda Brought You Home - Toni Braxton 22. Last Night - Az Yet 23. Someone to Love - Jon B. ft. Babyface 24. Never Forget You - Mariah Carey 25. Melt Away - Mariah Carey 26. When You Believe - Whitney Houston & Mariah Carey 27. Count on Me - Whitney Houston & CeCe Winans 28. Let It Flow - Toni Braxton 29. You are Not My Kind of Girl - New Edition 30. Two Occasions - The Deele 31. Girlfriend - Pebbles 32. The Color of Love - Boyz II Men 33. I am Ready - Tevin Campbell 34. We Are Not Making Love No More - Dru Hill 35. Two Occasions - The Deele 36. A Song for Mama - Boyz II Men 37. Til You Do Me Right- After 7 38. Why- 3T 39. Never Gonna Let You Go- Faith Evans 40. Lets Get The Mood Right - Johnny Gill Si Mbaya Kujua .*Mjombaako* *©️BantuKwanza*
❤️ 👍 2

Comments