Deputy Government Spokesperson ~Mwanaisha Chidzuga
Deputy Government Spokesperson ~Mwanaisha Chidzuga
February 22, 2025 at 04:33 PM
Leo nilihudhuria hafla ya Madhrasatu DAARUSSALAAM iliyoko eneo wadi la Tiwi Mwachema Kaunti ya Kwale. Niliwasihi wazazi wakuze watoto kwa misingi ya dini ili wazidi kuwa na imani. "Nawasihi wazazi wenzangu tuweze kusisitiza watoto wetu waweze kusoma dini kwani tutakuwa tumewekeza Imani katika kizazi cha Kesho." Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mbali mbali wakiwemo viongozi wa kidini pamoja na maafisa wa ngazi za juu katika kaunti ya Kwale.

Comments