Tanzania ECD Network
Tanzania ECD Network
February 6, 2025 at 06:07 AM
**KIKAO CHA KIKOSI KAZI CHA TAIFA CHA TATHMINI NA USIMAMIZI WA UTEKELEZAJI WA PJT-MMMAM** Dodoma, 5 Februari 2025 Kikosi Kazi cha Taifa cha Tathmini na Usimamizi wa Utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM), kinachojumuisha Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN), Children in Crossfire (CiC), Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), pamoja na wadau wengine muhimu, kimekutana jijini Dodoma kufanya tathmini ya utekelezaji wa programu hii katika ngazi ya mkoa na halmashauri. PJT-MMMAM inalenga watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 8—kipindi muhimu sana kwa ukuaji na ujifunzaji katika maisha ya binadamu. Mpango huu unalenga kuhakikisha kwamba watoto wanapata malezi na makuzi sahihi ili kufanikisha ukuaji timilifu na maendeleo endelevu. Katika kikao hiki, wajumbe wa kikosi kazi walijadili mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizopo, na mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa PJT-MMMAM. Ripoti za tathmini zimeonyesha maendeleo makubwa, hususan katika ushirikiano kati ya wadau, huku zikibainisha maeneo yanayohitaji kuboreshwa kwa ufanisi zaidi wa programu hii. Vikao vya mapitio kwa robo ya Oktoba–Desemba 2024 vinaendelea kufanyika mwezi Februari 2025, lengo likiwa ni kuboresha zaidi utekelezaji wa PJT-MMMAM katika ngazi zote. Kikosi kazi kimeazimia kuendelea kushirikiana kwa karibu na serikali pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha malengo ya programu yanatimia na watoto wa Tanzania wanapata malezi bora yanayostahili.
❤️ 1

Comments