
Tanzania ECD Network
70 subscribers
About Tanzania ECD Network
Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN) is a national umbrella Network of Early Childhood Development (ECD) Civil Society Organizations working to promote Early Childhood Development in Tanzania to children aged 0 to 8 yeqrs by influencing change in policies, programmes and practices. Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN) was founded in December 2000. Our Contact Details Area D-Mlimwa East Plot Number 30 Block K, Dodoma, P.O Box 4104, Dodoma, Tanzania. +255 753 882 954 | +255 755 446 540 [email protected] | [email protected] Website: www.tecden.or.tz
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

**KIKAO CHA KIKOSI KAZI CHA TAIFA CHA TATHMINI NA USIMAMIZI WA UTEKELEZAJI WA PJT-MMMAM** Dodoma, 5 Februari 2025 Kikosi Kazi cha Taifa cha Tathmini na Usimamizi wa Utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM), kinachojumuisha Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN), Children in Crossfire (CiC), Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), pamoja na wadau wengine muhimu, kimekutana jijini Dodoma kufanya tathmini ya utekelezaji wa programu hii katika ngazi ya mkoa na halmashauri. PJT-MMMAM inalenga watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 8—kipindi muhimu sana kwa ukuaji na ujifunzaji katika maisha ya binadamu. Mpango huu unalenga kuhakikisha kwamba watoto wanapata malezi na makuzi sahihi ili kufanikisha ukuaji timilifu na maendeleo endelevu. Katika kikao hiki, wajumbe wa kikosi kazi walijadili mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizopo, na mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa PJT-MMMAM. Ripoti za tathmini zimeonyesha maendeleo makubwa, hususan katika ushirikiano kati ya wadau, huku zikibainisha maeneo yanayohitaji kuboreshwa kwa ufanisi zaidi wa programu hii. Vikao vya mapitio kwa robo ya Oktoba–Desemba 2024 vinaendelea kufanyika mwezi Februari 2025, lengo likiwa ni kuboresha zaidi utekelezaji wa PJT-MMMAM katika ngazi zote. Kikosi kazi kimeazimia kuendelea kushirikiana kwa karibu na serikali pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha malengo ya programu yanatimia na watoto wa Tanzania wanapata malezi bora yanayostahili.

*Timu ya Uratibu wa PJT-MMMAM Zanzibar Yatembelea TECDEN* Timu ya uratibu wa uanzishaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) Zanzibar imefanya ziara ya mafunzo ya siku tatu Tanzania Bara kwa lengo la kujifunza kuhusu uandaaji, uratibu, na utekelezaji wa programu hiyo. Ziara hiyo ilihusisha wajumbe kutoka Afisi ya Rais - Ikulu, Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, pamoja na wadau kama Save the Children na D-tree. Katika ziara hiyo, timu ilitembelea TECDEN, mshirika muhimu katika uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika utekelezaji wa afua za Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Hatua hii inaendana na agizo na maono ya Mhe. Dkt. Hussein Ally Mwinyi, Rais wa Zanzibar, ya kuimarisha mifumo ya malezi Makuzi na maendeleo ya watoto nchini. #ECDTanzania #TECDEN #MaleziNaMakuzi #WatotoKwanza

Februari 13-14, 2025, TECDEN iliandaa mkutano wa wadau wa huduma za malezi ya wa miaka 0-5 katika Hoteli ya Seashells, Dar es Salaam, kujadili hali utoaji huduma za malezi ya watoto, kwa ufadhili wa Global School Forum. Mkutano huu uliwakutanisha wadau wa sekta binafsi kujadili mafanikio, changamoto, na fursa za kuboresha huduma za malezi ya watoto nchini Tanzania. Majadiliano yalilenga kutafuta suluhisho bora, jumuishi, na endelevu katika sekta hii ili kusaidia upatikanaji wa huduma bora kwa watoto wa wazazi wanaofanya kazi. #MaleziBora #MaleziCampaign

*Vikao vya Sekretarieti ya Uratibu wa PJT-MMMAM – Februari 19-20, 2025* Tarehe 19-20 Februari 2025, Sekretarieti ya Uratibu wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) iliendelea na vikao vyake vya kila mwezi kwa lengo la kupitia maendeleo na kujadili masuala muhimu ya utekelezaji wa programu hii. Mjadala ulijikita katika masuala ya kitaifa, ukisisitiza uwajibikaji, matumizi sahihi ya takwimu katika maamuzi, na mshikamano wa kisekta, kuendelea kufanya tafiti mbalimbali ili kuhakikisha kila mtoto anapata huduma bora za malezi, malezi, makuzi na maendeleo ya awali. Tumekubaliana kuimarisha uratibu, kuhamasisha rasilimali, na kuhakikisha utekelezaji thabiti wa mpango huu kwa ustawi wa watoto na maendeleo ya taifa. TECDEN inaendelea kuchangiza utekelezaji wa masuala ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ili kuhakikisha kila mtoto anapata huduma stahiki. #PJT-MMMAM #Uwajibikaji #UshirikianoKisekta #MaleziMakuzi #MaleziCampaign

*Uwasilishaji wa PJT-MMMAM- Mkoa wa Shinyanga* Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la ICS imefanya uwasilishaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kwenye kikao cha tathmini ya maendeleo ya elimu kilichofanyika Kahama. Kikao hiki kilihudhuriwa na washiriki kutoka idara ya elimu, wakuu wa shule, wamiliki wa shule binafsi, wamiliki wa vituo vya daycare, benki, NGOs, Wabunge, na Madiwani. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe: Anamringa Macha. Lengo ni kuongeza uelewa, bajeti na ushirikiano katika kuimarisha malezi, Makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto mkoani Shinyanga. PJT-MMMAM inalenga kuhakikisha kuwa watoto wote Tanzania wenye umri wa miaka 0 hadi 8 wapo kwenye mwelekeo sahihi wa kufikia ukuaji timilifu kwa kupata huduma jumuishi za Afya, Lishe, ulinzi na usalama, Malezi yenye mwitikio na fursa za ujifuzaji wa awali. #Mtotokwanza #MaleziCampaing #WekezakwaWatoto #PJT-MMMAM

*Uongozi wa Kimageuzi na Mabadiliko ya Utamaduni kwa Maendeleo ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto* Kuanzia tarehe 25 hadi 26 Februari, Tanzania ECD Network kwa kushirikiana na Spark Health Africa imeendesha mafunzo maalum kwa viongozi wakuu ili kuharakisha utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Kitaifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) 2021/22-2025/26. Mafunzo haya yalilenga: ✅ Kuimarisha uwajibikaji na maamuzi sahihi kwa maendeleo ya malezi na makuzi ya awali ya mtoto ✅ Kukuza imani na ushirikiano wa sekta mbalimbali ili kuongeza athari chanya ✅ Kuboresha uratibu na uongozi kwa utekelezaji bora wa mpango wa kitaifa ✅ Kutetea upangaji wa bajeti na mgao wa rasilimali kwa watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 8 Mafunzo haya yaliwaleta pamoja viongozi wakuu kutoka wizara husika—Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Waziri Mkuu, na Wizara ya Afya—pamoja na viongozi wa ngazi ya mkoa, Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya na Waganga Wakuu wa Wilaya kutoka Chamwino, Kongwa, Bahi, na Jiji la Dodoma. Kwa pamoja, tunawekeza katika mustakabali ambako kila mtoto anastawi kwa kupata rasilimali na huduma stahiki kwa maendeleo yao! #UongoziBoraKwaWatoto #PJTMMMAM #WekezaKwaMtoto #MaleziCampaign #MakuziBora