
Tanzania ECD Network
February 12, 2025 at 09:53 AM
*Timu ya Uratibu wa PJT-MMMAM Zanzibar Yatembelea TECDEN*
Timu ya uratibu wa uanzishaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) Zanzibar imefanya ziara ya mafunzo ya siku tatu Tanzania Bara kwa lengo la kujifunza kuhusu uandaaji, uratibu, na utekelezaji wa programu hiyo.
Ziara hiyo ilihusisha wajumbe kutoka Afisi ya Rais - Ikulu, Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, pamoja na wadau kama Save the Children na D-tree. Katika ziara hiyo, timu ilitembelea TECDEN, mshirika muhimu katika uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika utekelezaji wa afua za Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto
Hatua hii inaendana na agizo na maono ya Mhe. Dkt. Hussein Ally Mwinyi, Rais wa Zanzibar, ya kuimarisha mifumo ya malezi Makuzi na maendeleo ya watoto nchini.
#ecdtanzania #tecden #malezinamakuzi #watotokwanza
👍
1