Tanzania ECD Network
Tanzania ECD Network
February 24, 2025 at 08:26 AM
*Vikao vya Sekretarieti ya Uratibu wa PJT-MMMAM – Februari 19-20, 2025* Tarehe 19-20 Februari 2025, Sekretarieti ya Uratibu wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) iliendelea na vikao vyake vya kila mwezi kwa lengo la kupitia maendeleo na kujadili masuala muhimu ya utekelezaji wa programu hii. Mjadala ulijikita katika masuala ya kitaifa, ukisisitiza uwajibikaji, matumizi sahihi ya takwimu katika maamuzi, na mshikamano wa kisekta, kuendelea kufanya tafiti mbalimbali ili kuhakikisha kila mtoto anapata huduma bora za malezi, malezi, makuzi na maendeleo ya awali. Tumekubaliana kuimarisha uratibu, kuhamasisha rasilimali, na kuhakikisha utekelezaji thabiti wa mpango huu kwa ustawi wa watoto na maendeleo ya taifa. TECDEN inaendelea kuchangiza utekelezaji wa masuala ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ili kuhakikisha kila mtoto anapata huduma stahiki. #pjt-MMMAM #uwajibikaji #ushirikianokisekta #malezimakuzi #malezicampaign
🙏 1

Comments