
Tanzania ECD Network
February 24, 2025 at 02:08 PM
*Uwasilishaji wa PJT-MMMAM- Mkoa wa Shinyanga*
Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la ICS imefanya uwasilishaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kwenye kikao cha tathmini ya maendeleo ya elimu kilichofanyika Kahama.
Kikao hiki kilihudhuriwa na washiriki kutoka idara ya elimu, wakuu wa shule, wamiliki wa shule binafsi, wamiliki wa vituo vya daycare, benki, NGOs, Wabunge, na Madiwani. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe: Anamringa Macha.
Lengo ni kuongeza uelewa, bajeti na ushirikiano katika kuimarisha malezi, Makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto mkoani Shinyanga.
PJT-MMMAM inalenga kuhakikisha kuwa watoto wote Tanzania wenye umri wa miaka 0 hadi 8 wapo kwenye mwelekeo sahihi wa kufikia ukuaji timilifu kwa kupata huduma jumuishi za Afya, Lishe, ulinzi na usalama, Malezi yenye mwitikio na fursa za ujifuzaji wa awali.
#mtotokwanza #malezicampaing #wekezakwawatoto #pjt-MMMAM
✅
👍
2