Tumainimedia
Tumainimedia
February 4, 2025 at 03:55 AM
LEO FEBRUARI 4 TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU GILBERTI (1190),PADRE NA MWANZILISHI WA SHIRIKA Gilberti alizaliwa Sempringham (Uingereza), siku za mwisho za utawala wa Mfalme Wiliam. Alikuwa mwana wa Joselini, ambaye alikuwa mkuu wa mji wa Sempringham, Joselini alimtuma Paris (Ufaransa) ili akasome huko. Akiwa Paris Gilberti alifuzu na aliporudi alianzisha shule huko Sempringham. Aliwafundisha watoto wa watu maskini jinsi ya kupata Utakatifu. Punde baba yake alimpa urithi kutoka katika mashamba yake mawili huko Sempringham. Gilberti aligawa karibu mali yote kwa maskini. Akivutiwa na fadhila zake, Askofu wa Lincoln alimpa Upadre ingawa Gilberti mwenyewe hakupenda sana. Baba yake alipokufa mwaka 1130, Gilberti aliondoka katika jumba la Askofu akaanza kuutumia urithi alioachiwa na baba yake. Alianzisha Monasteri mbili peke yake. Moja ilikuwa ya Masista waliofuata kanuni ya Wabenediktini na nyingine ilikuwa ya wanaume waliojiita Wagilberti, wakafuata kanuni ya Mtakatifu Augustino nao walidumu mpaka wakati mfalme Henriko wa Nane alipojitenga na Kanisa Katoliki. Wakati ule zilipatikana Monasteri Ishirini na sita za Wagilberti. Mtakatifu Gilberti alipata taabu nyingi. Mabruda wake walimshitaki kwa Papa, wakati mwingine alishitakiwa, ati kwa kutoa msaada kwa Toma wa Becket (tunayemkumbuka 29 Disemba) aliyekuwa uhamishoni. Hii ilikuwa uongo, lakini kwa sababu hiyo alitupwa gerezani. Baadaye, aliupinga uongozi wa shirika lake hilo na alifurahi kujiondoa na kuishi tu maisha ya kawaida ya jumuiya. Moja ya desturi zake ilikuwa kuweka mezani pake sahani aliyoiita 'Sahani ya Bwana Yesu' ambamo aliweka sehemu nzuri zaidi ya chakula chake kwa ajili ya maskini. Mtakatifu Gilberti alikufa Mwaka 1190 akiwa na Umri wa Miaka 104 Alikuwa ameliomba Shirika lake litoe misaada mingi kwa watu maskini na wenye ukoma. Alitangazwa kuwa Mtakatifu Mwaka 1202. MTAKATIFU GILBRETI PADRE NA MWANZILISHI WA SHIRIKA UTUOMBEE. #tumainimedia
🙏 1

Comments