
Tumainimedia
88 subscribers
About Tumainimedia
Watie moyo nduguzo
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

LEO FEBRUARI 15 TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU WALFRIDO, ABATI (765) Walfrido alizaliwa Pisa (Italia). Alioa Mwanamke ambaye alimpenda sana, wakazaa watoto wa kiume watano na mmoja wa kike. Baadaye, Walfrido na Mkewe Tesia walisikia moyoni kuwa Mungu anawaita waingie Utawani. Walikuwa na marafiki wawili wenye ndoa ambao walikuwa na tamaa hiyo hiyo. Walikutana wakajadiliana juu ya maisha yao ya baadaye. Walichagua mlima mmoja wakajenga juu yake nyumba ya watawa wanaume. Kutoka hapo kwenda mwendo wa saa tano kwa miguu wakajenga Konveti kwa ajili ya wanawake. Konventini humo wake zao na binti mmoja wa Walfrido wakavikwa shela ya utawa. Utawa huu mpya uliwavutia watu wengi waingie na baada ya kupita miaka michache idadi ya Wamonaki iliongezeka kuwa sitini, kati yao akiwamo Gimfrido, mtoto wa Walfrido. Gimfrido alifanywa kuwa Padre lakini alipata kishawishi kikubwa akatoroka Utawani pamoja na watu wengine akachukua pia farasi na hati zilizokuwa mali ya jumuiya. Walfrido aliona uchungu sana, akasali akimwomba Mungu amrudishe mwanae Gimfrido na kumpa alama itakayokuwa kumbukumbu yake maisha yake yote. Siku hiyo hiyo Gimfrido alikamatwa na kurudishwa utawani akiwa ametubu makosa yake. Lakini kidole cha kati cha mkono wake wa kuume kilikuwa kimeharibika vibaya sana hata hakuweza kukitumia tena. Mtakatifu Walfrido alisimamia Monasteri kwa hekima kwa miaka kumi na alipokwisha kufa mwanae Gimfrido alirithi wadhifa wake, akawa Padre mwema na mashuhuri. MTAKATIFU WALFRIDO, ABATE UTUOMBEE. #tumainimedia #tumainitv

https://youtu.be/WioPUjY4eVo?si=bGFi1um5jFqMXVxv KARIBU TUSALI PAMOJA MISA YA LEO JUMATATU ASUBUHI.

LEO FEBRUARI 10 2025 TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MT.SKOLASTIKA, MTAWA (547) Skolastika alikuwa dada pacha wa Mtakatifu Benedikto (tunayemkumbuka11 Julai). Walizaliwa huko Norsia (Italia)Mwaka 480 wote wawili walijitolea kwa Mungu. Walipokufa walizikwa katika kaburi moja Mtakatifu Benedikto alipojenga Monasteri ya Monte Kasino, Skolastika alikuja kukaa karibu apate kufuata kanuni za Wabenediktini. Kila mwaka ndugu na umbuye walikutana katika nyumba moja, nje yao ili wapate kusimuliana mambo ya Mungu na furaha kubwa za mbingu. Walipokutana mara ya mwisho Skolastika alitamani sana kusikiliza mafundisho ya Benedikto, hata siku moja jua lilipoanza kutua, alimsihi nduguye asiondoke Lakini Benedikto alimgombeza akisema: "Haifai hata kidogo wamonaki kulala nje ya Monasteri yao". Basi Skolastika alianza kumwomba Mungu amzuie ndugu yake asiondoke. Alifunga mikono, aliinamisha kichwa chake mezani akasali kwa bidii na kutoa machozi. Mungu alisikiliza maombi yake, Kwa ghafula yalikuja mawingu meusi na ngurumo ilisikika na umeme ukametameta na ghafla mvua ilianza kunyesha kwa nguvu sana. Benedikto alishindwa kabisa kuondoka Akasema: "Mungu akusamehe, dada; je, umefanya nini?" Skolastika akajibu: "Nilikuomba ubaki hapa, nawe ukakataa. Nikamwomba Mungu naye akanikubalia". Wote wawili wakazungumza maneno ya Mungu usiku kucha. Siku tatu baada ya hayo Benedikto aliona roho ya dada yake Skolastika ikipaa uwinguni mfano wa njiwa, Ilikuwa mwaka 547 Alimshukuru Mungu Benedikto alitwaa maiti ya dada yake akaizika. Kisha siku arobaini Benedikto naye alikufa akazikwa humo humo katika kaburi la dada yake. MTAKATIFU SKOLASTIKA MTAWA UTUOMBEE. #tumainimedia #tumainitv

LEO PIA FEBRUARI 14 MAMA KANISA ANAMKUMBUKA MTAKATIFU VALENTINO, PADRIE Februari 14 ni Siku ya "Valentine Day" asili yake ni kutoka Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (Memoria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake Sikukuu ya Daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padre Valentino aliyeuawa na utawala wa Kirumi. Mtakatifu Valentini alizaliwa mwaka 226 AD huko Terni, Nchini Italia na aliuawa Februari 14, 269 AD huko Roma, Italia. Aliuawa kwa sababu ya kutetea Waamini wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu. Lakini sikukuu hiyo imeenea sana katika nchi za Magharibi na baadaye karibu sehemu kubwa ya Ulimwengu huisherehekea kama siku ya Mapenzi kinyume cha dhamira ya Mtakatifu Valentine. Watawala wa dola ya kirumi walikuwa na fikra za kueneza Dola ya Kirumi duniani kote na hivyo Vijana hawakutakiwa kuoa ili wawe huru muda wote kwenda vitani kupigania nchi. Hii ilimaanisha kuwa kama wangeoa wasingekuwa na uhuru wa kwenda Vitani bali kuwa na familia zao. Vijana wengi wakawa na mtindo wa kuwa na vimada tu kitu ambacho Kanisa lilikuwa linapinga. Padre Valentino ambaye alikuwa Roma, akawa anawahimiza vijana kufunga ndoa badala ya kufanya ngono bila ndoa, kwani ni dhambi na kitu kisichokubalika mbele za macho ya MUNGU. Akawa anafungisha ndoa kwa siri kubwa kwenye Makatakombe yaani Mahandaki chini ya Kanisa ambako kuna sehemu za Ibada kwa watu wachache na alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka Amri ya Wakuu wa Dola ya Kirumi. Baadhi ya watu walifichua siri hiyo hivyo Padre Valentino alishikwa na uongozi wa Dola ya Warumi na kuuawa kama Shahidi Mfiadini kwa ajili ya kutetea Waamini wake wafunge ndoa badala ya maisha ya ngono zembe bila ndoa. Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume kote Ulimwenguni, likatenga tarehe maalum ya kumkumbuka Padre Valentino kama mfiadini sababu ya kutetea maisha ya Wanakanisa kuwa wanandoa. Ni tarehe14, Februari kila mwaka. Baadaye ikapokeleka na watu hata wasio na imani ya Kikristo kama ni siku ya kufanya kumbukumbu kwa Mtakatifu Valentino kama mtetezi wa Ndoa. Maudhui ya siku hiyo kwa wasio Wanakanisa imechukua maana nyingine ya kwamba ni siku ya wapendanao hata kwa wasio wanandoa ilimradi wanapendana, kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya Mfia Dini Mtakatifu Padre Valentino aliyetaka vijana wafunge ndoa badala ya kuwa na hawara tu (vimada). Wenye hofu ya MUNGU tunaalikwa kuiheshimu Siku hii kama ni Siku Takatifu ya kumpendeza MUNGU kwa watu tuwapendao na sio kuifanya kama siku ya kutenda machukizo mbele ya MUNGU. Tumuombe Mtakatifu Valentino, Padre atuombee kwa MUNGU tuwe na upendo wa kweli kwa watu tuwapendao ili hatimaye tutimize mapenzi ya MUNGU wetu. "PENDANENI KAMA NILIVYOWAPENDA NINYI" MTAKATIFU VALENTINE. UTUOMBEE #tumainimedia

https://youtu.be/z7uYwUUfgmM MISA TAKATIFU LEO IJUMAA ASUBUHI.

LEO FEBRUARI 4 TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU GILBERTI (1190),PADRE NA MWANZILISHI WA SHIRIKA Gilberti alizaliwa Sempringham (Uingereza), siku za mwisho za utawala wa Mfalme Wiliam. Alikuwa mwana wa Joselini, ambaye alikuwa mkuu wa mji wa Sempringham, Joselini alimtuma Paris (Ufaransa) ili akasome huko. Akiwa Paris Gilberti alifuzu na aliporudi alianzisha shule huko Sempringham. Aliwafundisha watoto wa watu maskini jinsi ya kupata Utakatifu. Punde baba yake alimpa urithi kutoka katika mashamba yake mawili huko Sempringham. Gilberti aligawa karibu mali yote kwa maskini. Akivutiwa na fadhila zake, Askofu wa Lincoln alimpa Upadre ingawa Gilberti mwenyewe hakupenda sana. Baba yake alipokufa mwaka 1130, Gilberti aliondoka katika jumba la Askofu akaanza kuutumia urithi alioachiwa na baba yake. Alianzisha Monasteri mbili peke yake. Moja ilikuwa ya Masista waliofuata kanuni ya Wabenediktini na nyingine ilikuwa ya wanaume waliojiita Wagilberti, wakafuata kanuni ya Mtakatifu Augustino nao walidumu mpaka wakati mfalme Henriko wa Nane alipojitenga na Kanisa Katoliki. Wakati ule zilipatikana Monasteri Ishirini na sita za Wagilberti. Mtakatifu Gilberti alipata taabu nyingi. Mabruda wake walimshitaki kwa Papa, wakati mwingine alishitakiwa, ati kwa kutoa msaada kwa Toma wa Becket (tunayemkumbuka 29 Disemba) aliyekuwa uhamishoni. Hii ilikuwa uongo, lakini kwa sababu hiyo alitupwa gerezani. Baadaye, aliupinga uongozi wa shirika lake hilo na alifurahi kujiondoa na kuishi tu maisha ya kawaida ya jumuiya. Moja ya desturi zake ilikuwa kuweka mezani pake sahani aliyoiita 'Sahani ya Bwana Yesu' ambamo aliweka sehemu nzuri zaidi ya chakula chake kwa ajili ya maskini. Mtakatifu Gilberti alikufa Mwaka 1190 akiwa na Umri wa Miaka 104 Alikuwa ameliomba Shirika lake litoe misaada mingi kwa watu maskini na wenye ukoma. Alitangazwa kuwa Mtakatifu Mwaka 1202. MTAKATIFU GILBRETI PADRE NA MWANZILISHI WA SHIRIKA UTUOMBEE. #tumainimedia

[01/02, 15:12] Fr. Henry Rimisho: SAUTI YA MTU ALIAYE NYIKANI…ITENGEZENI njia ya BWANA yanyoosheni Mapito yake… ( Math 3:3) JUMAPILI YA 4 MWAKA -C- (2.02.2025) “Jubilee 2025, Mahujaji wa MATUMAINI” MASOMO: Somo la I: . Yer 1:4-5,17-19 Somo la II: 1Kor 12:31; 13:1-13 Somo injili: .Lk 4:21-30 UTANGULIZI: Masomo haya yanatufundisha kwamba Mungu anatuita kwa kazi yake na anatupa nguvu. Tunapaswa kuishi kwa upendo wa kweli, na tusimfungie Mungu ndani ya matarajio yetu binafsi. Tuombe neema ya kumtambua na kumpokea Mungu katika maisha yetu ya kila siku, hata pale tunaposhawishika kumsukumia mbali kama watu wa Nazareti walivyofanya. SOMO la KWANZA: Yeremia 1:4-5, 17-19 Katika SOMO hili, Mungu anamwita nabii Yeremia na kumhakikishia kuwa alimteua kabla hajazaliwa. Pia anamwambia asihofu, kwani atampa nguvu za kusimama imara mbele ya watu, hata kama watampinga. Katika SOMO la KWANZA tunajifunza Jambo (1) lifuatalo: 1.WİTO wa MTUMISHI WA MUNGU: Huu ni ujumbe wa faraja kwa yeyote anayejisikia mdogo au hafai kwa kazi ya Mungu. Yeremia katika umri wake mdogo anaitwa na Mungu kuwa NABII, wito huu unajawa na changamoto nyingi kutokana na umri. Lakini Mungu anampigania hili kufikia lengo lake. Hivyo, Kila mmoja wetu ana mwito wa pekee, na Mungu hatuachi peke yetu tunapokabiliana na changamoto za utume wetu. SOMO la PILI: 1 Wakorintho 12:31 – 13:1-13 Katika SOMO la PILI tunajifunza Jambo (1) lifuatalo: 1.UPENDO wa KWELI na ŞIFA ZAKE: Mtume Paulo anatufundisha kuwa kipaji kikuu kuliko vyote ni upendo. Bila upendo, hata matendo makubwa ya imani hayana maana. Anabainisha sifa za upendo wa kweli: hustahimili, hauna wivu, haujisifu, haukasiriki kwa urahisi, na hufurahia ukweli. Hili ni somo muhimu kwa jamii zetu leo. SWALI: Tunawezaje kuwa mashahidi wa upendo huu katika familia, jumuiya, na mahali pa kazi? SOMO la INJILI TAKATIFU: Injili: Luka 4:21-30 Yesu anahubiri kwa watu wa Nazareti, lakini badala ya kumpokea kwa furaha, wanamkataa kwa sababu walimjua tangu utoto wake. Anawaambia kuwa hakuna nabii anayekubalika katika nchi yake, jambo linalowakera hadi wanataka kumuua. Hii ni changamoto kwetu pia. SWALI: Je, tunapuuza ukweli kwa sababu ya ubaguzi au mazoea? SWALI: Je, tunakataa ukweli wa Mungu unapokuja kupitia watu au hali tusizozitarajia? Katika SOMO la INJILI TAKATIFU İnatufundisha mambo Makuu (4) yafuatayo: 1. YESU ATANGAZA KWA UJASIRI: “LEO MAANDIKO HAYA YAMETIMIA” Hii ni kauli nzito sana kwa watu waliomsikiliza. Wanashangazwa na hekima yake lakini bado wanabaki na mashaka. Wanashindwa kumwelewa kwa sababu wanamwona kama kijana wa kawaida waliyekua naye. Wapendwa,hii ni changamoto kubwa kwa kila mmoja wetu: je, tunamruhusu Mungu atufikie kwa njia zisizotarajiwa? Watu wa Nazareti walimchukulia Yesu kwa mtazamo wa kibinadamu pekee, kuwa ni mwana wa Yusufu. Hivyo wakashindwa kutambua utukufu wake. Hata sisi tunaweza kumpuuza Mungu anapotuongea kupitia watu tunaodharau au hali tunazoziona kuwa za kawaida. 2. “DOKTA, JIPONYEE MWENYEWE” – WATU WANAMASHAKA NA YESU Baada ya Yesu kusema kuwa maandiko yametimia, watu wanamwelekea kwa mashaka na Yesu. Hii ni aina ya imani inayotaka kuona kwanza ndipo iamini. Watu wa Nazareti wanataka uthibitisho wa macho badala ya kuwa na imani ya kweli. Lakini Yesu anawakataa kwa sababu imani ya kweli haihitaji uthibitisho wa ishara tu, bali unyenyekevu wa moyo unaopokea ukweli wa Mungu. Wapendwa,Imani yetu haipaswi kutegemea tu kuona miujiza. Watu wengi leo wanakimbilia unabii na ishara badala ya kujenga uhusiano wa kweli na Mungu. Yesu anatufundisha kuwa imani ya kweli ni kumwamini Mungu hata pale tunapokosa kuona ishara za haraka. 3. YESU AWAKUMBUSHA ISRAELI JINSI WAGENI WALIVYOPOKELEWA NA MUNGU Yesu anawapa mifano miwili kutoka Agano la Kale: 1. Eliya na mjane wa Sarepta (1Fal 17:8-16) – Kulikuwa na njaa Israel, lakini Mungu hakumtuma Eliya kwa wajane wa Israeli, bali kwa mwanamke Mpagani huko Sarepta. 2. Elisha na Naamani (2Fal 5:1-14) – Ingawa Israeli walikuwa na watu wengi wenye ukoma, nabii Elisha alimponya Naamani, jemadari wa kigeni kutoka Aramu. Kwa mifano hii, Yesu anaonyesha kuwa mara nyingi wale waliodhaniwa kuwa “wa mbali” na Mungu ndio waliopokea neema kwa sababu walifungua mioyo yao kwa imani. Wapendwa,Mungu hatabiriki wala hajifungi kwa taifa moja au kundi fulani. Wana wa Israeli walijiona kuwa watu wa Mungu pekee, lakini Yesu anaonyesha kuwa hata watu wa mataifa walihitaji wokovu na waliupokea kwa imani. SWALI: Je, sisi tunajiona kuwa tuko karibu sana na Mungu kiasi cha kuwadharau wengine? Mungu anaweza kutumia mtu yeyote, hata yule tunayemdharau, kutuletea ujumbe wake wa wokovu. 4. WATU WAMKATAA YESU NA WANATAKA KUMUUA Baada ya Yesu kusema haya, watu wa Nazareti wanachukia sana. Wanasukumwa na hasira, wanamsukuma hadi kwenye mwinuko wa mlima ili wamtose chini na kumuua. Kwao, Yesu amevuka mipaka kwa kuwalinganisha na wale waliomkataa Mungu katika historia. Lakini maandiko yanasema: “Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.” Hili linaonyesha kuwa hawakuwa na mamlaka juu yake. Wakati wake wa kufa haukuwa umefika, na maisha yake yalikuwa mikononi mwa Mungu. Wapendwa, Yesu anakataliwa kwa sababu alisema ukweli ambao watu hawakutaka kuusikia. Hii inatufundisha kuwa mara nyingi, ukweli wa Mungu unaweza kupingwa, na wale wanaousimamia wanaweza kupata upinzani mkali. Kama wafuasi wa Kristo, hatupaswi kuogopa kusimamia ukweli hata kama tunapingwa. HITIMISHO: UNABII HAUKUBALIKI KWA WAO WENYEWE Yesu anatoa somo kuu: “Hakuna nabii anayekubalika kwao wenyewe.” Hili linatufundisha kuwa mara nyingi tunashindwa kutambua na kuthamini kazi ya Mungu ndani ya watu tuliowazoea. Watu wa Nazareti walimjua Yesu kama mwana wa seremala, wakadhani hawawezi kupokea wokovu kupitia kwake. MASWALI YA KUJIHOJI: 1. Je, ninamruhusu Mungu kuniongelesha kupitia watu au njia nisizotarajia? 2. Je, ninamwamini Mungu hata pale ambapo sioni ishara za haraka? 3. Je, nina moyo wa unyenyekevu wa kupokea ukweli wa Mungu hata kama unaniweka kwenye changamoto? 4. Je, naweza kuendelea kushuhudia imani yangu hata nikipata upinzani? SALA: Ee Bwana Yesu, unayetufundisha kuwa nabii hapokelewi katika nchi yake, tusaidie tusiwe na mioyo migumu kama watu wa Nazareti. Utufungue macho tuweze kukutambua katika maisha yetu ya kila siku na tukupokee kwa imani ya kweli. Amina. TUMSIFU YESU KRISTU🙏🏾 Tafakari hii imeandaliwa nami, Rev. Fr. Henry Rimisho AJ (Kwa msaada wa Roho Mtakatifu) [01/02, 17:30] Fr. Henry Rimisho: SAUTI YA MTU ALIAYE NYIKANI…ITENGEZENI njia ya BWANA yanyoosheni Mapito yake… ( Math 3:3) DOMINIKA YA SIKUKUU YA KUTOLEWA BWANA HEKALUNI. JUMAPILI YA 4 MWAKA -C- (2.02.2025) “Jubilee 2025, Mahujaji wa MATUMAINI” MASOMO: Somo I: 3:1-4 Somo II: 2:14-15 Injili: Lk 2:22-40 UTANGULIZI: Sikukuu ya Kutolewa kwa Bwana Yesu Hekaluni ni tukio lenye uzito wa pekee katika fumbo la ukombozi. Yesu, akiwa bado mchanga, anapelekwa Hekaluni kama inavyotakiwa na Torati, lakini kwa undani zaidi, tendo hili linaashiria kujitoa kwake kwa Mungu na kwa wanadamu. Tukio hili linatuonyesha jinsi Mungu anavyotimiza ahadi zake kwa njia ya Yesu Kristo. SOMO LA KWANZA: Somo la Kwanza: Malaki 3:1-4 Nabii Malaki anatabiri kuja kwa Mjumbe wa Agano, ambaye ataitakasa hekalu na watu wake. Yesu ndiye utimilifu wa unabii huu, kwani Yeye ni Mwanga wa Mataifa na utakaso wa waamini. Katika SOMO la KWANZA linatufundisha Jambo (1) lifuatayo: 1.UTAKASO WA MUNGU Somo linatufundisha kuwa Mungu hututakasa kupitia Kristo, hivyo tunaalikwa sote tujikabidhi kwa Mungu Baba kwa kuwa anatarajia nasi kujitoa kikamilifu kwake hili kutimiza Ahadi zake. SOMO la PILI: Waebrania 2:14-18 Katika SOMO la PILI tunajifunza Jambo (1) lifuatalo: 1.YESU AMEUVAA UBINADAMU WETU: Mtume Paulo anasisitiza kuwa Yesu alishiriki hali yetu ya kibinadamu ili apate kutushinda na kutuokoa kutoka utumwa wa dhambi na mauti. Kwa kujitoa kwake, anatufanya kuwa ndugu zake wa kweli, akituonyesha kuwa tunapaswa kuwa tayari kujitoa kwa Mungu na kwa wengine. SOMO LA INJILI TAKATIFU: Injili: Luka 2:22-40 Maria na Yosefu wanampeleka Yesu Hekaluni ili kumtolea kwa Mungu, wakitimiza sheria ya Kiyahudi. Katika tukio hili, tunakutana na Simeoni na Ana, watu wa imani kubwa waliokuwa wakingoja kwa hamu wokovu wa Mungu. Simeoni anampongeza Mungu kwa sababu amemwona Masiya kabla ya kufa. Maneno yake yanaonyesha kuwa Yesu ni “Mwanga wa Mataifa” na “Utukufu wa Israeli.” Ana pia anamshuhudia Yesu kama ukombozi wa watu wa Mungu. Katika SOMO la INJILI TAKATIFU tunajifunza mambo Makuu (4) yafuatayo: 1.YESU NI MWANGA WA MATAIFA. Yesu alikuja kuwa nuru kwa ulimwengu mzima. Kama Wakristo, tunaitwa kuwa mwanga kwa wengine kwa maisha yetu ya imani, upendo, na haki. Tunapaswa kumruhusu Yesu kutakasa maisha yetu ili tuwe mashahidi wa nuru yake. 2.KUJITOA KWA MUNGU. Yesu, pamoja na wazazi wake, anajitoa kwa Mungu Hekaluni. Hili linatufundisha umuhimu wa kujitoa kwa Mungu bila masharti. Hili linajidhihirisha kwa namna tunavyoishi maisha ya sala, unyenyekevu, na huduma kwa wengine. 3.IMANI NA SUBIRA YA SIMEONI NA ANNA. Simeoni na Anna walimngoja Masiya kwa muda mrefu kwa imani thabiti. Subira yao ni mfano mzuri wa jinsi tunavyopaswa kuendelea kumtumainia Mungu hata tunapopitia changamoto. Mungu daima hutimiza ahadi zake kwa wakati wake. 4.KRISTO KAMA CHEMCHEM YA WOKOVU. Yesu anapotolewa Hekaluni, anatufundisha kuwa wokovu wetu unapatikana kwa kumkabidhi Mungu maisha yetu kikamilifu. Tunapaswa kushiriki kikamilifu katika maisha ya Kanisa, sakramenti, na matendo ya huruma. HITIMISHO Sikukuu hii ni mwaliko wa kujitoa kwa Mungu bila masharti kama Yesu alivyofanya. Tunapaswa kuwa mwanga kwa wengine kwa matendo yetu mema na kushikilia imani hata katika nyakati ngumu. SWALI: Je, tuko tayari kumruhusu Yesu atakase maisha yetu na kutufanya vyombo vya nuru yake kwa ulimwengu? Bwana atupe neema ya kujitoa kwake kikamilifu, ili nasi tuwe mwanga kwa wengine. Amina. Ninawatakia MAPADRE, WATAWA wa kike na wanaume wote katika KANISA, HERİ NA BARAKA ya Sikukuu ya kutolewa kwa BWANA HEKALUNI. TUMSIFU YESU KRISTU🙏🏾 Tafakari hii imeand aliwa nami, Rev. Fr. Henry Rimisho AJ (Kwa msaada wa Roho Mtakatifu) #Tumaini Media

LEO FEBRUARI 5, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU AGATHA, BIKIRA NA MFIADINI (251) Agatha alikuwa Msichana wa jamaa bora, nzuri na tajiri. Basi, Kwinsiano, Gavana wa Sisilia, alitamani sana kumwoa kwa sababu ya uzuri wake. Agatha alikataa kishujaa akisema kwamba amekwisha olewa na Mchumba mwingine, yaani Yesu Kristo Mwana wa Mungu mwenyewe. Kwinsiano kusikia hayo alikasirika sana. Basi, aliamuru watesi wamtese vikali. Waliyakata maziwa ya Agatha kwa nguvu na kumlaza mzima juu ya makaa ya moto, Nchi ilitetemeka. Kwinsiano alikimbia, maana Watu walimkasirikia wakisema kuwa Mungu anaiadhibu Nchi kwa sababu ya ubaya wake. Agatha alirudishwa gerezani na mara alizamia Roho. Mwaka mmoja baada ya hayo Mlima Etna ulitoa moto, Nchi yote karibu ingeteketea. Lakini Watu wa Etna walimkimbilia Mwenyeheri kwenye kaburi la Agatha, walitwaa shela, wakaielekeza upande wa mlima uliokuwa ukitokota moto. Mara moto ulizimika na watu wa Etna waliokoka. Ndiyo sababu Mtakatifu Agatha huheshimiwa sana katika Italia yote. MTAKATIFU AGATHA, BIKIRA NA MFIADINI, UTUOMBEE.