Tumainimedia
Tumainimedia
February 5, 2025 at 09:06 AM
LEO FEBRUARI 5, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU AGATHA, BIKIRA NA MFIADINI (251) Agatha alikuwa Msichana wa jamaa bora, nzuri na tajiri. Basi, Kwinsiano, Gavana wa Sisilia, alitamani sana kumwoa kwa sababu ya uzuri wake. Agatha alikataa kishujaa akisema kwamba amekwisha olewa na Mchumba mwingine, yaani Yesu Kristo Mwana wa Mungu mwenyewe. Kwinsiano kusikia hayo alikasirika sana. Basi, aliamuru watesi wamtese vikali. Waliyakata maziwa ya Agatha kwa nguvu na kumlaza mzima juu ya makaa ya moto, Nchi ilitetemeka. Kwinsiano alikimbia, maana Watu walimkasirikia wakisema kuwa Mungu anaiadhibu Nchi kwa sababu ya ubaya wake. Agatha alirudishwa gerezani na mara alizamia Roho. Mwaka mmoja baada ya hayo Mlima Etna ulitoa moto, Nchi yote karibu ingeteketea. Lakini Watu wa Etna walimkimbilia Mwenyeheri kwenye kaburi la Agatha, walitwaa shela, wakaielekeza upande wa mlima uliokuwa ukitokota moto. Mara moto ulizimika na watu wa Etna waliokoka. Ndiyo sababu Mtakatifu Agatha huheshimiwa sana katika Italia yote. MTAKATIFU AGATHA, BIKIRA NA MFIADINI, UTUOMBEE.
🙏 1

Comments