
Tumainimedia
February 10, 2025 at 04:25 AM
LEO FEBRUARI 10 2025 TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MT.SKOLASTIKA, MTAWA (547)
Skolastika alikuwa dada pacha wa
Mtakatifu Benedikto (tunayemkumbuka11 Julai). Walizaliwa huko Norsia (Italia)Mwaka 480 wote wawili walijitolea kwa Mungu.
Walipokufa walizikwa katika kaburi moja Mtakatifu Benedikto alipojenga Monasteri ya Monte Kasino, Skolastika alikuja kukaa karibu apate kufuata kanuni za Wabenediktini.
Kila mwaka ndugu na umbuye walikutana katika nyumba moja, nje yao ili wapate kusimuliana mambo ya Mungu na furaha kubwa za mbingu.
Walipokutana mara ya mwisho Skolastika alitamani sana kusikiliza mafundisho ya Benedikto, hata siku moja jua lilipoanza kutua, alimsihi nduguye asiondoke Lakini Benedikto alimgombeza akisema: "Haifai hata kidogo wamonaki kulala nje ya Monasteri yao".
Basi Skolastika alianza kumwomba Mungu amzuie ndugu yake asiondoke. Alifunga mikono, aliinamisha kichwa chake mezani akasali kwa bidii na kutoa machozi.
Mungu alisikiliza maombi yake, Kwa ghafula yalikuja mawingu meusi na ngurumo ilisikika na umeme ukametameta na ghafla mvua ilianza kunyesha kwa nguvu sana.
Benedikto alishindwa kabisa kuondoka Akasema: "Mungu akusamehe, dada; je, umefanya nini?" Skolastika akajibu: "Nilikuomba ubaki hapa, nawe ukakataa. Nikamwomba Mungu naye akanikubalia". Wote wawili wakazungumza maneno ya Mungu usiku kucha.
Siku tatu baada ya hayo Benedikto aliona roho ya dada yake Skolastika ikipaa uwinguni mfano wa njiwa, Ilikuwa mwaka 547
Alimshukuru Mungu Benedikto alitwaa maiti ya dada yake akaizika.
Kisha siku arobaini Benedikto naye alikufa akazikwa humo humo katika kaburi la dada yake.
MTAKATIFU SKOLASTIKA MTAWA UTUOMBEE.
#tumainimedia
#tumainitv
🙏
1