Tumainimedia
Tumainimedia
February 18, 2025 at 07:34 AM
LEO FEBRUARI 18, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU TEOTONI, ABATE (1166) Teotoni alikuwa Padre mwenye maisha Matakatifu na hakupenda raha za dunia. Alikuwa pia Mhubiri hodari ambaye sifa zake zilienea mbali katika Nchi ya Ureno. Aliwapenda sana maskini na Roho za Marehemu toharani, ambao aliwaombea kila Ijumaa kwa kuimba Misa ya wafu. Baada ya Misa, aliongoza maandamano kwenda makaburini na watu wote walimfuata. Wakati ule Malkia wa Ureno alikuwa Mjane, lakini alikuwa akitembea na Mwanaume mmoja. Siku moja wote wawili walikuwapo Kanisani wakati Padre Teotoni alipohubiri kwa maneno makali. Ilionekana wazi kuwa yalikuwa yanawaelekea wao. Waliyaona haya, na mawazo yao yakachafuka sana hivi kwamba wakatoka upesi Kanisani. Safari nyingine Malkia huyo alimpelekea ujumbe kabla ya Misa, akimwomba afupishe kidogo muda wa Ibada. Padre Teotoni akampelekea Malkia ujumbe akisema kwamba alikuwa anatolea sadaka ya Misa kwa heshima ya Mfalme wa Mbinguni ambaye ni Mkuu kuliko Binadamu yeyote wa ukoo wa Kifalme hapa duniani. Akaongeza kuwa Malkia ana uhuru kamili wa kukaa au kuondoka. Malkia alijawa majuto, akamngoja mpaka Ibada ilipokwisha, ndipo akaenda kumwomba radhi Mtakatifu na kupokea maonyo yake. Padre Teotoni aliingia baadaye Utawani na huko akawa Abate, Aliishi humo miaka 30 ya mwisho ya Maisha yake, akafa akiwa na umri wa miaka 80. MTAKATIFU TEOTONI, ABATI, UTUOMBEE. #tumainitv #tumainimedia

Comments