GEORGE AMBANGILE
GEORGE AMBANGILE
February 16, 2025 at 10:59 AM
#playmaker | Ederson kwenye majukumu ya De Bruyne na Rodri Analyst @sistiinho 👉 Kwenye post ya Jan 29 niliandika kuhusu mbinu za Man City kupita juu ya kuta za uzuiaji za wapinzani wao baada ya ku-attract Presha; 1. Wapinzani wakizuia vyema Man City kupita katikati ya kuta zao za uzuiaji (Passing Through The Press/Block) kwakutumia viungo wa kati 2. Wapinzani wao wakizuia vyema Man City kupita pembeni ya kuta zao za uzuiaji (Passing Around The Press/Block) kwakutumia wachezaji wa pembeni Full-Backs/Wings 👉 Kwenye njia ya juu tukaona namna Man City wanavyofaidika na uwezo wa kiufundi wa wachezaji wao kama; 1. Ederson ambaye hupiga mipira mirefu inayoangukia nyuma ya mstari wa mwisho wa uzuiaji wa wapinzani 2. Halaand ambaye hushambulia space nyuma ya wapinzani au hulengwa na mipira kutoka kwa Ederson 👉 LAKINI kwenye chapisho la February 8 baada ya Newcastle kuwakanda Arsenal 2-0, nilielezea ubora wa Newcastle kiuzuiaji chini ya Eddie Howe ambapo nilielezea ubora wao ku-MASTER njia za wapinzani wao; 1. Kimfumo/ muundo (4-5-1, 5-4-1) 2. Style (high, mid, low block/press) 3. Njia (katikati, pembeni na Juu) 👉 Lakini leo MAN CITY wametumia silaha muhimu kuweza kunasuka kwenye mitego yote ya NEWCASTLE kwa kutumia silaha hizi; 1. Kumtumia Ederson kama FREE PLAYMAKER hasa kupita juu pindi Newcastle wanapokuwa wamefanya MAN MARKING na kuzuia vizuri njia za juu ambapo Ederson aliwasaidia City; - Kuwa mchezaji wa ziada kwenye build up structure ya City dhidi ya Pressing Structure ya Newcastle (Numerical Superiority) - Kuwa na uwezo wa kiufundi kutumia pasi yake moja kujenga na kuendeleza shambulizi, kupenya kuta za uzuiaji za Newcastle, na kutengeneza nafasi ya kufunga jukumu ambalo lingefanywa na combination ya wachezaji wengi (Qualitative Superiority) - Kuweka mipira nyuma ya ukuta wa Newcastle kurahisisha kazi ya utengenzaji (Positional Superiority) 2. Mawasiliano ya Halaand na Marmoush - Mmoja akikimbia kurudi kwao na kumtengenezea mwingine urahisi kushambulia space akiwa na beki mmoja (1v1) - Mmoja huweza kuwa kama Target man na ku-link shambukizi kwa mwingine Hilo ni goli moja kati ya manne ya Marmoush leo Man City 4-0 Newcastle. Enjoy
👍 🫡 ❤️ 🔥 😎 🙏 🫶 28

Comments