GEORGE AMBANGILE WhatsApp Channel

GEORGE AMBANGILE

8.7K subscribers

About GEORGE AMBANGILE

Football Analyst Wasafi Media Supersport Swahili Commentator Betway Brand Influencer

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

GEORGE AMBANGILE
GEORGE AMBANGILE
2/10/2025, 9:21:35 AM
โค๏ธ ๐Ÿ‘ ๐Ÿ”ฅ โšฝ ๐Ÿ˜ข 17
Video
GEORGE AMBANGILE
GEORGE AMBANGILE
2/10/2025, 9:21:36 AM

PEDRI 1: Uzito wa pasi zake ( zinafika mahala sahihi , kwa wakati sahihi na kumrahisishia mpokeaji ) 2: Anajua mazingira yanayomzunguka nini kinaendelea ( ina mrahisishia kufanya maamuzi sahihi mara nyingi kuliko mara chache anazokosea ) 3: Anajua kuchagua spaces sahihi ambazo :- โœ๐ŸปZinasaidia kwenye kipindi cha kuisogeza timu juu ( Progression ) โœ๐ŸปZinampa nafasi ya kupeleka matatizo kwa mpinzani 4: Hazidishi vitu katika utendaji wake ( ana rahisisha mchezo )

โค๏ธ ๐Ÿ‘ ๐Ÿ”ฅ ๐Ÿซก ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ™ ๐Ÿค ๐Ÿ“Œ ๐Ÿ˜ฎ ๐Ÿฅ‚ 62
GEORGE AMBANGILE
GEORGE AMBANGILE
2/16/2025, 10:59:50 AM
๐Ÿ‘ โค๏ธ 4
Video
GEORGE AMBANGILE
GEORGE AMBANGILE
2/16/2025, 10:59:57 AM

#Playmaker | Ederson kwenye majukumu ya De Bruyne na Rodri Analyst @sistiinho ๐Ÿ‘‰ Kwenye post ya Jan 29 niliandika kuhusu mbinu za Man City kupita juu ya kuta za uzuiaji za wapinzani wao baada ya ku-attract Presha; 1. Wapinzani wakizuia vyema Man City kupita katikati ya kuta zao za uzuiaji (Passing Through The Press/Block) kwakutumia viungo wa kati 2. Wapinzani wao wakizuia vyema Man City kupita pembeni ya kuta zao za uzuiaji (Passing Around The Press/Block) kwakutumia wachezaji wa pembeni Full-Backs/Wings ๐Ÿ‘‰ Kwenye njia ya juu tukaona namna Man City wanavyofaidika na uwezo wa kiufundi wa wachezaji wao kama; 1. Ederson ambaye hupiga mipira mirefu inayoangukia nyuma ya mstari wa mwisho wa uzuiaji wa wapinzani 2. Halaand ambaye hushambulia space nyuma ya wapinzani au hulengwa na mipira kutoka kwa Ederson ๐Ÿ‘‰ LAKINI kwenye chapisho la February 8 baada ya Newcastle kuwakanda Arsenal 2-0, nilielezea ubora wa Newcastle kiuzuiaji chini ya Eddie Howe ambapo nilielezea ubora wao ku-MASTER njia za wapinzani wao; 1. Kimfumo/ muundo (4-5-1, 5-4-1) 2. Style (high, mid, low block/press) 3. Njia (katikati, pembeni na Juu) ๐Ÿ‘‰ Lakini leo MAN CITY wametumia silaha muhimu kuweza kunasuka kwenye mitego yote ya NEWCASTLE kwa kutumia silaha hizi; 1. Kumtumia Ederson kama FREE PLAYMAKER hasa kupita juu pindi Newcastle wanapokuwa wamefanya MAN MARKING na kuzuia vizuri njia za juu ambapo Ederson aliwasaidia City; - Kuwa mchezaji wa ziada kwenye build up structure ya City dhidi ya Pressing Structure ya Newcastle (Numerical Superiority) - Kuwa na uwezo wa kiufundi kutumia pasi yake moja kujenga na kuendeleza shambulizi, kupenya kuta za uzuiaji za Newcastle, na kutengeneza nafasi ya kufunga jukumu ambalo lingefanywa na combination ya wachezaji wengi (Qualitative Superiority) - Kuweka mipira nyuma ya ukuta wa Newcastle kurahisisha kazi ya utengenzaji (Positional Superiority) 2. Mawasiliano ya Halaand na Marmoush - Mmoja akikimbia kurudi kwao na kumtengenezea mwingine urahisi kushambulia space akiwa na beki mmoja (1v1) - Mmoja huweza kuwa kama Target man na ku-link shambukizi kwa mwingine Hilo ni goli moja kati ya manne ya Marmoush leo Man City 4-0 Newcastle. Enjoy

๐Ÿ‘ ๐Ÿซก โค๏ธ ๐Ÿ”ฅ ๐Ÿ˜Ž ๐Ÿ™ ๐Ÿซถ 28
GEORGE AMBANGILE
GEORGE AMBANGILE
2/19/2025, 9:56:32 AM
๐Ÿ‘ โค๏ธ ๐Ÿ‘Š 5
Image
GEORGE AMBANGILE
GEORGE AMBANGILE
2/19/2025, 9:56:33 AM

Wakati Antonio Conte yupo Spurs kwenye press conference alikumbushia kwamba wakati yupo Italia alikuwa na rafiki yake mmoja ambaye ni Mkurugenzi wa Michezo anaitwa Pantaleo Corvino . Pantaleo aliwahi kumuambia Conte kwamba " Unaweza kukosea kuhusu Mke lakini sio mshambuliaji na golikipa" Muktadha ni katika kujenga timu , Golikipa na Straika ni sehemu ambazo hutakiwi kukosea . Binafsi nakubali kabisa tena ongeza na namba 6 . Lakini tubakie hapo kwanza kwenye GK na Straika. โœ๐ŸปUkiacha majukumu yao MAMA ( Gk = Kuokoa , mpira usiingie wavuni . Straika = kufunga magoli ) โœ๐ŸปLakini pia siku hizi wana umuhimu mkubwa sana pale timu zao zikiwa na umiliki wa mpira hasa kwenye uanzishwaji wa mashambulizi / ujenzi wa uchezaji kuanzia nyuma ( Build up ) . Katika hii miaka kama miwili hivi umuhimu ndio umeongezeka zaidi kwanini ? 1: Kwasababu siku hizi Ulaya timu nyingi sana zina ujasiri wa kukabia juu zaidi kwa staili ya " Man to Man high pressing = Man oriented pressing " yani kwamba kila mtu na wake kuanzia juu ya uwanja kabisa 2: Hii ilikuwa mara nyingi timu kubwa zinafanya sana dhidi ya timu ambazo wanazimudu kiubora wa wachezaji lakini siku hizi haipo tena hiyo 3: Hata timu za kawaida haziogopi kufanya hivyo dhidi ya timu kubwa na bora Ulaya , ujasiri umeongezeka na unatoka kwa makocha ndio wanasisitiza mno . Sasa hapo ndio inakuja umuhimu wa GK & Straika ambao inabidi wawe na sifa zifuatazo kukabiliana na man to man high pressing GOLIKIPA โœ๐ŸปUpigaji pasi mzuri ambao una sifa zaidi ya moja ( Passing range ) : Pasi fupi & ndefu uwiano sahihi . Kwenye hii kesi basi pasi ndefu za GK ndio silaha kubwa ( Mfano Ederson ) 2: STRAIKA โœ๐ŸปHapa kuna aina mbili ya straika wenye sifa tofauti : Kuna yule ambaye mzuri sana goli kalipa mgongo ( Drogba , Diego Costa , Ibrahimovic , Giroud , Kane , Benzema etc etc ) na wale ambao wazuri sana kushambulia space zilizowazi ( Haaland , Isak , Watkins ) au washambuliaji wa pembeni kama Salah , Mbappe etc Fanya Man to Man pressing dhidi ya timu yenye GK na Straika wenye sifa kama hizo utajionea rangi . Mpira mmoja tu mbele unapata adhabu stahiki .!

๐Ÿ‘ โค๏ธ ๐Ÿ”ฅ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜… ๐Ÿ™Œ ๐Ÿ™ ๐Ÿค ๐Ÿซก ๐Ÿซถ 27
GEORGE AMBANGILE
GEORGE AMBANGILE
2/23/2025, 12:38:52 PM
โค๏ธ ๐Ÿ‘ 2
Video
GEORGE AMBANGILE
GEORGE AMBANGILE
2/23/2025, 12:38:55 PM

#Tactics | Real Madrid Attacking Princples under Carlo Ancelotti Analyst @sistiinho Hizi ni mbinu za kushambulia za Real Madrid zilizowapa magoli matatu dhidi ya Man City; ๐Ÿ‘‰ 1st Clip; Passing through the Press - Goli la pili la Real Madrid limetokea kwenye moment Madrid wakiwa wanajenga shambulizi kuanzia langoni kwao (Building up from back) huku Man City wakizuia kwa shinikizo kubwa kuanzia mbele (High Pressing) 1. Build up structure ya Madrid ilikuwa na muundo wa 3+4 kutoka kwenye mfumo wa 4-2-3-1, kipa Courtous akiwa katikati ya mabeki wake wawili, Asensio na Rudigar 2. Pressing Structure ya Man City ilikuwa kwenye umbo la 4-1-2-1-2 (mfumo wa 4-4-2) - Lengo la Madrid kuanzia nyuma ni ku-attract pressure ya City ili watengeneze depth kubwa ya uzuiaji na kuacha nafasi katikati au nyuma ya pressing structure yao. - Madrid waliweza kutoka kirahisi kwenye pressure ya City kwasababu walikuwa wamewazidi idadi kwenye kila phase, yaani; 1. Build up phase ilikuwa 3v2; Courtous, Asensio na Rudigar vs Savinho na Marmoush 2. Build up Progression phase 4v1; Katikati Tchoumeni na Ceballos walikuwa dhidi ya Gundogan, ikawa rahisi kwa Madrid ku-progess kwao (Central Progerssion) au Valverde na Mendy pembeni (Wide Progressions). - Madrid walitumia wide combinations kufunga wakifaidika na Triangle ya pembeni, ambapo; 1. Valverde alishambulia channel ya pembeni nje 2. Rodrigo aliingia kwenye channel ya ndani 3. Bellingham akiwa nyuma ya viungo wa City - Triangle hii iliweza kupenya na kutengeneza nafasi kirahisi kwa kugongeana pasi za haraka na Bellingham na Rodrigo kubadilishana nafasi haraka, Bellinghma alishambulia half-space na Rodrigo kushambulia Zone 14 na kutengeneza nafasi kwa Mbappe ๐Ÿ‘‰ 2nd Clip; Passing Over the Press - Goli la kwanza la Madrid limetokea kwenye moment Madrid wakiwa na Mpira huku Man City wakizuia na Mid Block, Madrid wailinga kwa kufaidika na; 1. Pressure ndogo ya City mbele iliyowaacha Madrid kuwa Creative 2. Space kubwa nyuma ya block ya Man City ambayo Mbappe aliishambulia - Pasi moja tu ya juu inamaliza kazi ๐Ÿ‘‰ 3rd Clip; Passing Around the Press - Goli la 3, Madrid walizuinguka Block ya City ikiwa Compact

๐Ÿ‘ โค๏ธ ๐Ÿ”ฅ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ™ ๐Ÿฅถ 28
Link copied to clipboard!