GEORGE AMBANGILE
GEORGE AMBANGILE
February 19, 2025 at 09:56 AM
Wakati Antonio Conte yupo Spurs kwenye press conference alikumbushia kwamba wakati yupo Italia alikuwa na rafiki yake mmoja ambaye ni Mkurugenzi wa Michezo anaitwa Pantaleo Corvino . Pantaleo aliwahi kumuambia Conte kwamba " Unaweza kukosea kuhusu Mke lakini sio mshambuliaji na golikipa" Muktadha ni katika kujenga timu , Golikipa na Straika ni sehemu ambazo hutakiwi kukosea . Binafsi nakubali kabisa tena ongeza na namba 6 . Lakini tubakie hapo kwanza kwenye GK na Straika. ✍🏻Ukiacha majukumu yao MAMA ( Gk = Kuokoa , mpira usiingie wavuni . Straika = kufunga magoli ) ✍🏻Lakini pia siku hizi wana umuhimu mkubwa sana pale timu zao zikiwa na umiliki wa mpira hasa kwenye uanzishwaji wa mashambulizi / ujenzi wa uchezaji kuanzia nyuma ( Build up ) . Katika hii miaka kama miwili hivi umuhimu ndio umeongezeka zaidi kwanini ? 1: Kwasababu siku hizi Ulaya timu nyingi sana zina ujasiri wa kukabia juu zaidi kwa staili ya " Man to Man high pressing = Man oriented pressing " yani kwamba kila mtu na wake kuanzia juu ya uwanja kabisa 2: Hii ilikuwa mara nyingi timu kubwa zinafanya sana dhidi ya timu ambazo wanazimudu kiubora wa wachezaji lakini siku hizi haipo tena hiyo 3: Hata timu za kawaida haziogopi kufanya hivyo dhidi ya timu kubwa na bora Ulaya , ujasiri umeongezeka na unatoka kwa makocha ndio wanasisitiza mno . Sasa hapo ndio inakuja umuhimu wa GK & Straika ambao inabidi wawe na sifa zifuatazo kukabiliana na man to man high pressing GOLIKIPA ✍🏻Upigaji pasi mzuri ambao una sifa zaidi ya moja ( Passing range ) : Pasi fupi & ndefu uwiano sahihi . Kwenye hii kesi basi pasi ndefu za GK ndio silaha kubwa ( Mfano Ederson ) 2: STRAIKA ✍🏻Hapa kuna aina mbili ya straika wenye sifa tofauti : Kuna yule ambaye mzuri sana goli kalipa mgongo ( Drogba , Diego Costa , Ibrahimovic , Giroud , Kane , Benzema etc etc ) na wale ambao wazuri sana kushambulia space zilizowazi ( Haaland , Isak , Watkins ) au washambuliaji wa pembeni kama Salah , Mbappe etc Fanya Man to Man pressing dhidi ya timu yenye GK na Straika wenye sifa kama hizo utajionea rangi . Mpira mmoja tu mbele unapata adhabu stahiki .!
👍 ❤️ 🔥 😂 😅 🙌 🙏 🤝 🫡 🫶 27

Comments