Zeelakudisi
Zeelakudisi
February 8, 2025 at 01:08 PM
NYUMBA INAYOCHEZEWA NA WACHAWI Kujua kama nyumba yako inachezewa na wachawi Nenda katika mmea wa mkunde pori. Taratibu, piga magoti kabla haujanzaa kuchimba mzizi wa mti huu utanuia manuizi ya kwanini unautaka mzizi huo. Baada ya manuizi utauchimba mzizi wa mmea huo pamoja na mti wake kisha utaondoa matawi yote pamoja na majani. Baada ya hapo utarudi nao kwako kisha utauweka sehemu ya wazi katika chumba unacholala. Hakikisha sehemu uliouweka mzizi huo unapakumbuka vizuri, (Usiweke alama ya aina yoyote sehemu ulipouweka)Sasa, unaweza kulala usiku na kuuacha hapo. Ikiwa Asubuhi utakuta umehamishwa hata kidogo kutoka sehemu ulipokuwepo basi fahamu kuna mchawi aliingia katika nyumba yako. Ikiwa utakuta haujatolewa sehemu ulipokuwepo basi fahamu kwa asilimia 90% hakuna mchawi alieingia katika nyumba yako.
👍 2

Comments