Sekretarieti ya Ajira
                                
                            
                            
                    
                                
                                
                                February 10, 2025 at 09:11 AM
                               
                            
                        
                            Makamu Mwenyekiti wa Ofisi ya Rais  Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Bw. Said Kamugisha ametembelea kituo cha usaili Chuo Cha Utawala wa Umma kilichopo Tunguu Zanzibar ili kujionea namna zoezi hilo linavyoendelea.
Katika ziara hiyo, Bw.Kamugisha aliambatana na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Bw.Mick Kiliba na alipata nafasi ya kuzungumza na wasailiwa ambapo aliwaasa kufanya vyema kwenye usaili.
"Mchakato huu ni wa haki na uwazi hivyo niwahakikishie wale wote watakaofanya vizuri watapangiwa kazi kulingana na idadi ya nafasi zilizopo" alisema.
Aidha, viongozi hao walikutana na msailiwa mwenye ulemavu wa macho ambaye alipewa vifaa maalum vilivyomuwezesha kufanya usaili wa kuandika.
                        
                    
                    
                    
                    
                    
                                    
                                        
                                            ❤️
                                        
                                    
                                        
                                            😂
                                        
                                    
                                        
                                            🙏
                                        
                                    
                                    
                                        3