Sekretarieti ya Ajira
Sekretarieti ya Ajira
February 10, 2025 at 02:18 PM
Mjumbe wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Kuhanwa ametembelea kituo cha usaili Shule ya Sekondari Kigoma na Shule ya Sekondari Buronge zilizopo Mkoani Kigoma kujionea namna usaili wa kada mbalimbali za ualimu unavyoendelea. Aidha, Bi. Kuhanwa alizungumza na wasailiwa na kuwaeleza juu ya fursa iliyopo ya kanzidata ambayo inadumu kwa muda wa mwaka mmoja ambapo wasailiwa watakao faulu katika usaili na kutopangiwa vituo vya kazi awali kutokana na ufinyu wa nafasi wasikate tamaa kwani wanayo nafasi ya kuwekwa kwenye kanzi data inayodumu kwa muda wa mwaka mmoja na nafasi zikipatikana wasailiwa waliopo kwenye kanzi data nao watapangiwa vituo vya kazi.
👍 ❤️ 🤝 4

Comments