
Sekretarieti ya Ajira
February 14, 2025 at 04:37 PM
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Zanzibar Bw. Khatibu Mwinyichande (Wa katikati) ameipongeza Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa kazi nzuri ya uendeshaji wa mchakato wa ajira nchini.
Kamishna Mwinyichande ametoa pongezi hizo alipotembelea ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma- Zanzibar.
"Kufanya kazi au kuajiriwa ni suala muhimu katika ustawi wa haki za binadamu duniani, na hivyo Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma itaendelea kuwa mdau muhimu wa Tume ya Haki za Binadamu" aliongeza.
Katika ziara hiyo Kamishna Mwinyichande alipokelewa na Kaimu Katibu Msaidizi wa Bw. Selemani Chihembe.
🙏
❤️
😁
🤔
6