
Nipashe Digital
February 27, 2025 at 05:51 PM
#nipashedigitaldata leo inakuletea takwimu za matumizi ya laini za simu nchini kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
TCRA inabainisha kuwa laini za simu zinatumika kwa mawasiliano ya binadamu (P2P) na mawasiliano ya vifaa na mitambo (M2M). Kwa kipindi cha miezi mitatu, idadi ya laini zilizosajiliwa imeongezeka kutoka milioni 80.7 (Septemba 2024) hadi milioni 86.8 (Desemba 2024), ongezeko la asilimia 7.7.
#nipashemwangawajamii #nipashedigital