Dr Nature
Dr Nature
February 13, 2025 at 08:02 AM
Jinsi ya Kula Usipate KITAMBI Wakati wa KUNYONYESHA Mama unayenyonyesha ni kundi muhimu kwa sababu unakula kwa ajili yako na mtoto. Lengo la unachokula kukusaidia - Kutibu majeraha baada ya kujifungua - ⁠Kurejesha afya yako - ⁠Kuzalisha maziwa yenye afya ya kutosha kwa ajili ya mtoto. Hakuna anayekula ili awe na kitambi lakini kutoka na kutokuwa na uelewaa.. Wengi wamejikuta wanafuga vitambi vikubwa vinavyowatesa maisha yote. Ili ufikie malengo hayo ya lishe kwa mama anayenyonyesha.. unatakiwa ule vyakula vyenye sifa mbili: - Wingi wa virutubisho - ⁠Wingi wa viondoa sumu ‘antioxidants’ Maziwa hayatengenezwi kwa wingi wa chakula ila VIRUTUBISHO Yaani unaweza ukala na kunywa macchupa makubwa ya uji na mtori. Lakini kama hakuna virutubisho vya kutosha utaambulia kitambi na maziwa hayatatoka Cha muhimu: - Epuka vyakula vinavyoleta kitambi kama nyama na hizo supu zake, mtori wa ndizi, - ⁠uji lishe nao ukinywa sanaaa unapata kitambi Kula kawaida chakula hai (yaani chakula ambacho kwa sehemu kubwa kinatokana na mimea katika uasili wake) lakini ongeza vitu hivi kwa kiasi vinaongeza maziwa yenye afya sanaaa bila kukuletea kitambi - vikiko 2 vya unga wa mbegu ya maboga kwa siku - Kunde za kupika - ⁠Nyanya chungu za kupika - ⁠pilipili manga Ni rahisi sana.. Hutahangaika na kitambi na wala njaa njaa za usiku kwa sababu ya kunyenyesha hautazisikia Rafiki yako, Dr Nature
🙏 1

Comments