Dr Nature
Dr Nature
February 18, 2025 at 06:16 AM
Mbogamboga zina wingi wa nyuzilishe na virutubisho ambavyo ni viondoa sumu mwilini ‘antioxidants’. Katika wiki jitahidi kutumia mbogamboga za aina tofuati. Ni muhimu kwa sababu kila kundi la mbogamboga lina faida zake za tofauti ambazo huwezi kuzipata kwa kundi lingine. Mboga za majani za kijani kibichi ni chakula chenye afya zaidi duniani. Zinakupatia virutubisho vingi zaidi kwa kila kalori kuliko aina nyingine yoyote ya chakula. Zinakusaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi kwa 20% pamoja na magonjwa mengine sugu. Kila unapoandaa na kupakua chakula, hakikisha angalau nusu ya Sahani yako inakuwa ni mbogamboga. Zipo za aina nyingi; • Kachumbari • Mboga za majani • Mbogamboga zingine kama karoti, nyanya chungu, bamia, bilinganya Nk • Jamii ya kabeji kama brokoli, kauliflawa, kabeji Kadri Sahani yako inavyokuwa na rangi za kupendeza ndivyo ambavyo kinakuwa chenye afya zaidi. Zile rangi za kuvutia za mbogamboga ndio ‘antioxidants’ yaani viondoa sumu vyenyewe. Rafiki yako, Dr Nature
❤️ 🙏 3

Comments