
Abuu Mus'ab Media
February 1, 2025 at 09:28 AM
*#sha'BAAN: FANYA HARAKA KULIPA SWAUM UNAYODAIWA YA RAMADHAN ILIYOPITA*
_*Miongoni mwa yanayowajibu kutanabahi pamoja na kuingia mwezi huu (wa Sha'baan) ni kuwa aliye na deni anayolazimika kuilipa ya Ramadhani iliyopita inamwajibu kufanya haraka kuilipa kabla Ramadhani haijaingia, basi ni juu ya baba na mume kumkumbusha mkewe na wanawe kulipa masiku yaliyowapita, hakika wengi miongoni mwa watu wanatasahal (wanachukulia sahali) na kujisahaulisha mpaka inawaingilia Ramadhani, basi yakawa matokeo ya huku kusema nitafunga nitafunga na kufanya tasahul ni kupata madhaambi na kutoa kafara.*_
[Khutba: Haa qadi stahalla sha'baan; ya Sheikh Khalid Adh-dhafiry-Allah amhifadhi]
الشيخ د. خالد بن ضحوي الظفيري حفظه الله:
مما يجب التنبيه عليه مع دخول هذا الشهر أن من كان عليه قضاء من رمضان الماضي فيجب عليه المبادرة إلى القضاء قبل دخول رمضان، فعلى الأب والزوج أن يذكر زوجته وأولاده بقضاء ما فاتهم، فإن كثيرا من الناس يتساهلون ويتناسون حتى يدخل عليهم رمضان فيترتب على هذا التسويف والتساهل الإثم والكفارة.
[خطبة له بعنوان: ها قد استهل شعبان]
════ ❁✿❁ ════
*Salafi Da'wah East Africa (Salafi Da'wah Afrika Mashariki)*