UFUNUO CHANNEL
UFUNUO CHANNEL
February 2, 2025 at 07:21 PM
_Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, akiwa na mhuri wa Mungu aliye hai... Ufunuo 7:2_ Katika Agano la Kale, pepo husimama badala ya nguvu angamizi azitumiazo Mungu ili kutekelezea hukumu juu ya waovu (Yer. 23:19, 20). Ni njia nyingine ya kuelezea mapigo saba ya mwisho yatakayomimiwa juu ya wanadamu wasiotubu mara tu kabla ya Marejeo (Ufunuo 16). Hata hivyo, nguvu hizi angamizi zinazuiwa kwa Mungu kuingilia kati wakati hatua ya kuwatia muhuri watu wa Mungu ikifanyika. Katika nyakati za zamani, maana ya msingi ya kutiwa muhuri ilikuwa umiliki. Maana ya kutiwa muhuri kiishara katika Agano Jipya ni kwamba “Bwana awajua walio wake” (2 Tim. 2:19). Mungu huwatambua watu Wake na kuwatia muhuri kwa Roho Mtakatifu (Efe. 1:13, 14; 4:30). Katika wakati wa mwisho, muhuri katika kipaji cha uso huwabainisha wale wanaochagua kuwa upande wa Mungu (Ufu. 14:1). Muhuri wa Mungu si alama inayoonekana iwekwayo kwenye kipaji cha uso wa mtu, bali humaanisha “kutulia katika kweli, kiakili na kiroho, kiasi kwamba hawawezi kuhamishwa.” Wale ambao, kwa kujua na kuridhia, wanajiunga na mnyama hupokea chapa ya mnyama (Ufu. 13:16, 17). Uaminifu wa watu wa Mungu waliotiwa muhuri umepimwa katika kila kizazi. Hata hivyo, kipimo cha uaminifu katika zahama ya mwisho kitakuwa utunzaji wa amri za Mungu (angalia Ufu. 12:17, 14:12).

Comments